Habari za Punde

Balozi Karume Atembelea Miundombinu ya Barabara Pemba na Kuwapongeza Wafanyakazi Kwa Kazi Yao Nzuri Kurudusha Huduma Hiyo kwa Wananchi.

Na mwandishi wetu
Waziri wa Ujenzi Mawasiliano na Uafirishaji Mhe.Balozi Ali Karume   amewataka wafanyakazi na wahandisi wa Wizara  hiyo kushirikiana  katika  kufanya uchambuzi na utafiti wa kina ili kuangalia mapungufu  yaliyojitokeza katika  miundombinu ya barabara kisiwani Pemba kwa lengo la kuepusha  uharibifu kwenye  miundombinu hiyo.

Amesema  wizara  ipo kwa  kufanya kazi kwa vitendo hiyo waendelee na nguvu waliyonayo  katika kuihudumia jamii kwa kurejesha mawasiliano ya barabara pale Inapoharibika,Balozi Karume ameyasema hayo katika kikao cha pamoja cha wahandisi wa wizara ya ujenzi mawasiliano na usafirishaji kisiwani Pemba.
Wakati wa kutathmini utendaji wa wizara katika kurejesha huduma ya miundombinu ya barabara na madaraja  yaliyoharibiwa na mvua kisiwani Pemba.
 .
Katika kikao hicho Katibu Mkuu wa wizara ya ujenzi  Mawasiliano na miundo mbinu Ndg.Mustafa Aboud Jumbe amewapongeza wahandisi hao kwa kuirudisha huduma ya mawasiliano kwa muda mfupi na wananchi  kuweza kuendelea na shughuli zao za kawaida .

Hata hivyo amelaumu ni kwa nini barabara zilizojengwa zimeharibika kabla ya miaka mitano na kuwapa muda wahandisi hao hadi Ijumaa kuelezea kwa kitaalamu kitu cha kufanya cha kurudisha mawasiliano kutoka katika sehemu zilizoharibika.

Naye Afisa Mdhamini wa wizara ujenzi  Mawasiliano na usafirishaji  Pemba Ndg.Hamad Ahmed Baucha  na muhandisi wa wizara hiyo wameahidi kuyafanyiakazi maagizo hayo kwa kuhakikisha wanayasimamia na kazi inaendelea kama ilivyopangwa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.