Habari za Punde

Mratibu wa Elimu Masafa Pemba Aagwa.
Kushoto aliekua mratibu wa elimu masafa Pemba Malim Haji Hamad Hassan (Mstaafu), katikati ni Mratibu wa Idara ya Mafunzo ya ualimu Pemba na kulia ni Malim Faki Sleyyum Faki


Maalim Haji Hamad Hassan akiwa na zawadi ambayo alikabidhiwa na Malim Mkubwa Ahmed Omar kwa niaba ya wafanya kazi wa idara ya mafunzo ya Ualimu Kisiwani Pemba

Na Ali Othman, Pemba

Mratibu wa Idara ya mafunzo ya ualimu Pemba Malim Mkubwa Ahmed Omar amewataka watendaji katika idara yake kuiga mfano wa aliekua mratibu wa mafunzo ya elimu masafa Pemba Maalim Haji Hamad Hassan ambae amestaafu rasmi hivi karibuni.

Akizungumza katika hafla fupi ya kumuaga aliekua Mratibu wa elimu masafa Pemba, Malim Mkubwa amempongeza kwa kufikia umri wa kustaafu akiwa na heshima kubwa kutokana na juhudi zake katika kusimamia majukumu yake. Amewaomba watendaji wengine katika idara hiyo kuiga mfano huo kwa kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwa bidii na juhudi kubwa.

Akitoa takwimu za wahitimu wa elimu masafa ambao walihitimu katika kipindi chake akiwa mratibu wa elimu masafa Pemba, Malim Haji amesema jumla ya wahitimu 805 wamehitimu mafunzo ya ualimu na kupatiwa vyeti kupitia elimu masafa kisiwani Pemba.

Wakati huo huo Mratimu wa mafunzo ya Ualimu kisiwani Pemba Malim Mkubwa Ahmed Omar amemkabidhi Mstaafu huyo zawadi ya Cherahani ambayo amezawadiwa na watendaji wa idara vikiwemo vituo vya walimu kisiwani Pemba. Ametoa historia yake nakusema kwamba, juhudi zake katika kazi zilianza tokea mwaka 1975 ambapo alianza kazi akiwa mwalimu katika skuli ya Kangagani. Ameongeza kwamba alitumikia nafasi hiyo ya kuelimisha hadi mwaka 2001 ambapo alipata nafasi ya Uratibu wa elimu masafa Pemba nafasi ambayo kwasasa inashikiliwa na Malim Hemed Said Masoud baada ya kustaafu kwake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.