Habari za Punde

Mvua za Masika Zinazoendelea Kunyesha Kisiwani Zanzibar.

Wananchi wakiwa upande wa pili wa barabara ya kwenda mwanakwerekwe wakiangalia jinsi mvua za masika zinavyonyesha na kujaa katika bwawa la mwanakwerekwe na maji hayo kuzuiya kupitika kwa barabara hiyo kutokana na kujaa maji na kutapakaa magugu maji.
Hii ndio barabara ya mwanakwerekwe ikiwa imefunikwa na maji ya mvua ilinyesha siku ya jumanne kutwa na kusababisha kuzuiya kutumika kwa barabara hii kutokana na kufurika maji katika barabara hiyo na maji ya magugu maji kutanda katika barabara hiyo kama inavyoonekana pichani.
1 comment:

  1. Assalaam alaykum. Jamaniii hili tatizo la Mwana kwerekwe naona kama Serikali yetu imesalimu amri vile, hakuna masika zilizosababisha madhara makubwa na usumbufu kwa wananchi kwa barabara hii.

    Jamani tumekosa mbinu mbadala kwa barabara hii ya Mwana kwerekwe?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.