Habari za Punde

Ziara ya Ujumbe wa Wadi ya Makunduchi Nchini Sweden.

Bi Fatma kutoka ujumbe wa Wadi ya Makunduchi akiwa na professa Katja kutoka idara ya jinsia katika Chuo kikuu cha Mid Sweden baada ya mazungumzo ya kutafuta ushirikiano wa kupambana ukatili dhidi ya wanawake Makunduchi. Aidha wadi ya Makunduchi inatafuta pia mafunzo ya Munda mfupi na mrefu katika maswali ya jinsia.
Ujumbe wa Wadi ya Makunduchi kutoka Kushiro Mohamed Muombwa, mratibu na mwalimu Hafith. Hapa tumekuja kuangalia ufugaji wa nyuki wa Ulaya. Hulu ndio mzinga wa nyuki unaotumiwa sana nchi za baridi. Ufugaji wa nyuki wa kisasa hivi sasa umepamba moto Makunduchi
Mratibu wa mashirikiano kati ya wadi ya Makunduchi na manispaliti ya Sundsvall ndugu Mohamed Muombwa baada ya mazungumzo na Profesa Katja kuhusu uwezekano wa kushirikiana na Chou kikuu cha Mid Sweden University katika maswali ya kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake Makunduchi. Upande wa kulia ni bi Christin Stromberg mratibu wa mashirikiano upande wa Sundsvall

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.