Habari za Punde

Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM afiwa na mama yake mzazi

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif  Ali Iddi akimfariji Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar  Ndugu Vuai Ali Vuai aliyefiwa na Mama yake Mzazi Bibi Mwanaisha Hassan Vuai aliyezikwa kijijini kwao Bwejuu Mkoa wa Kusini Unguja.
 Waumini wa Dini ya Kiislamu wakimsalia Bibi Mwanaisha Hassan Vuai katika Msikiti wa Ijumaa Bwejuu aliyefariki Dunia jana katika Hospitali ya Global alipokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.

 Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu na Viongozi wa Serikali na Kisiasa wakimuombea Dua Marehemu Bibi Mwanaisha Hassan Vuai baada ya kumsalia kwenye Msikiti wa Ijumaa wa Bwejuu Mkoa Kusini Unguja.
 Baadhi ya Waumini wa Dini ya Kiislamu na Viongozi wa Serikali na Kisiasa wakimuombea Dua Marehemu Bibi Mwanaisha Hassan Vuai baada ya kumsalia kwenye Msikiti wa Ijumaa wa Bwejuu Mkoa Kusini Unguja.
Balozi Seif Ali Iddi kushoto akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Kusini Unguja Nd. Ramadhan Abdullah  Ali wakati wa msiba wa Mama Mzazi wa Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Zanzibar hapo Bwejuu Mkoa Kusini Unguja.

Picha na – OMPR – ZNZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.