Na Salmin Juma, Pemba
Zaidi ya wakulima 300 katika bonde la
Ukele Wilaya ya Micheweni huenda wakakosa kuvuna zao la mpunga baada ya
mashamba yao kuingia majichumvi yaliyochanganyika na maji ya mvua zinazoendelea
kunyesha na kusababisha kuvunja tuta na kuingia katika mashamba hayo.
Baadhi ya wakulima hao wamesema awali
walikuwa na matumaini ya kuvuna lakini baada ya kuingia maji chumvi
imesababisha kilimo hicho kuungua
Akizungumza na wakulima hao Naibu
waziri wa nchi ofisi ya makamo wa pili wa rais Mh Mihayo Juma Mhnunga amesema
Serikali tayari wameshaiona athari hiyo na hivi sasa wanatafuta njia ya
kuliboresha tuta hilo ili wakulima wasiathirike zaidi
Ameshauri kuwekwa mlango wa dharura
wa kusaidia kutoa maji hayo katika mashamba na kurejesha udongo uliochukuliwa
na maji ili wale waliokuwa hawajafikwa na maafa hayo wapate fursa ya kuvuna
mpunga wao.
Wakati huo huo Mh Mihayo ametembelea
barabara ya Gando eneo la Mangwena lililokatika wa mvua na kuwapongeza
wafanyakazi kwa kurejesha huduma ya usafiri kwa haraka licha ya uhaba wa vifaa
walivyonavyo.
Aidha Naibu waziri huyo ameshuhudia
ugawaji wa misaada ya chakula na nguo kwa wananchi waliopatwa na maafa katika
majimbo ya Kojani na Micheweni na kuwataka kuwa na umoja na mashirikiano pale
wanapokutwa na maafa .
No comments:
Post a Comment