Habari za Punde

Wazazi watakiwa kushirikiana na walimu kuhakikisha mtoto anapata elimu bora

Na Salmin Juma, Pemba

Wazazi na walezi watoto kisiwani Pemba wametakiwa kutoa mashirikiano ya kutosha baina yao na walimu ili kumfanya mtoto kupata elimu itakayomuokoa katika maisha yake duniani na akhera.

Tafiti zinaonyesha kuwa wananchi mbalimbali nchini zinaonyesha kua wanafunzi wengi hushindwa kufanya vizuri katika masomo kutokana na kutokuwepo kwa mashirikiano mazuri baina ya pande hizo mbili .

Akizungumza na mwandishi wetu Mwalim msaidizi wa madarasatul siraji-munira ya Kilindi wilaya ya chakechake Ust: Ramadhan Juma Ramadhan amesema kuwa, kuna baadhi ya wazazi hawatoi kabisa mashirikiano kwa maustadh pindi wanapowapeleka watoto wao chuoni.

Ust: Ramadhan amesema, ili kumfanya mtoto afanikiwe kielimu basi ni lazima kuwe na mashirikiano ya mzazi mwalimu na mtoto wenyewe.

 "tatizo kubwa ni msharikiano tu, inapotokea sote tunakua pamoja maendeleo makubwa yatapatikana kwa vijana wetu" amesema ust: Ramadhan

Nae Ust: Khelef Haroub Abdallah wa madrasatul- Nurul-islamiya ya Shingi mjini chakechake ameungana na ust: Ramadhani kwa kusema kua hakuna jambo kubwa linalorudisha nyuma maendeleo ya madarasa kama kutokuwepo mashirikiano baina wazazi na walimu kwa watoto wao.

Kwa upande wake Ust  Said Abdulrahman Muhammed    wa madrasatul   Khairia islamia  amesema "utandawazi uliyoingia nchini umechangia kiasi kikubwa kwa wazazi kutotoa mashirikiano kwa walimu" alisema Muhammed.

Pandu Juma Zaid ambae ni mzazi kutoka Msingini Chakechake amesema  kuna baadhi ya wazazi hawapotayari kutoa mashrikiano kwa walimu, amesema kufanya hivyo kunarudisha nyuma sana maendeleo ya watoto.

Ametoa wito kwa wazazi kutilia mkazo suala la elimu, huku wakijua kua wanapompatia elimu bora mtoto ndio mafanikio katika dunia na akhera.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.