Habari za Punde

CHAMA CHA UOKOAJI MAJINI TANZANZIA, CHAMA CHA MAKOCHA WA KUOGELEA NA KIKOSI CHA KMKM WANDAA MAFUNZO YA USALAMA MAJINI ZANZIBAR

Mmoja wa washiriki wa mafunzo ya usalama majini akimunyesha mgeni rasmin jinsi ya kutoa huduma ya kwanza kwa mtu alieza na kuokolewa katika mafunzo hayo.
Katibu Mkuu Chama cha Uokoaji majini Tanzania Ndg.Alexander Mwaipasi akitoa maelezo ya mafunzo ya usalama majini yatayofundishwa kwa muda wa wiki katika Skuli ya kimataifa iliyopo Mazizini Mjini Zanzibar
Kapten Khatibu Khamis wa Kikosi cha KMKM Zanzibar akifungua mafunzo ya usalama majini kwa vikundi mbalimbali vinavyojishuhulisha na uokoaji Afika Mashariki pamoja na skari wa jeshi hilo katika Skuli ya kimataifa Mazizini Mjini Zanzibar. (kulia) Katibu Mkuu chama cha uokoaji majini Tanzania Bwa. Alexander Mwaipasi na (kushoto) ni Katibu wa KMKM Sports Club luteni Sheha Mohammed Khamis
Mkufunzi Job Kania kutoka chama cha uokoaji cha Dunia (ILS) akifafanua jambo kwa baadhi ya wanafunzi wa mafunzo ya usalama majini yaliyofanyika Skuli ya kimataifa Mazizini Mjini Zanzibar. Picha na Makame Mshenga.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.