Habari za Punde

Hat Trick mbili zapigwa Pemba wakati Jamhuri ikiifunga Mwenge katika 8 bora Ligi Kuu 5-3

 Mchezaji wa Timu ya Mwenge Abdul Yussuf akiondoka na mpira baada ya kupiga Hatrick. Hata hivyo Timu ya Mwenge ilipoteza mchezo wake na Jamhuri kwa kufungwa 5-3
Mchezaji wa Timu ya Jamhuri Mwalimu Mohammed akiondoka na mpra baada ya kupiga Hat Trick wakati Timu yake ya Jamhuri ilipoifunga Timu ya Mwenge  jumla ya magoli 5-3. Magoli matatu yalifungwa na Mwalimu Mohammed 


Na: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.

Mshambuliaji wa timu ya Jamhuri Mwalimu Mohammed leo amefanikiwa kufunga mabao 3 (Hat trick) katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora na timu yake Jamhuri iliposhinda mabao 5-3 dhidi ya Mwenge kwenye mchezo uliopigwa jioni ya leo katika uwanja wa Gombani Pemba.

Mabao hayo amefunga katika dakika ya 11, 15, 27 ambapo katika mchezo huo huo mshambuliaji wa timu ya Mwenge Abdull Yussuf nae amelipa hat trick baada ya kufunga mabao yote 3 ya Mwenge katika mchezo huo waliopoteza mabao ambayo alifunga dakika ya 33, 37 na 79.

Washambuliaji hao wote wawili kwasasa ndio vinara wa kuzifumania nyavu katika ligi hiyo ambapo wote wakiwa na jumla ya mabao 7 kila mmoja wakifuatiwa na Ibrahim Hamad Hilika wa Zimamoto mwenye mabao 6 baada ya leo kufunga bao moja timu yake ilipotoka sare ya 1-1 dhidi ya JKU kwenye uwanja wa Amaan.

Jumla ya Hat trick tatu mpaka sasa zimeshafungwa katika ligi hiyo zikiwemo mbili za leo pamoja na ya wiki iliyopita iliyofungwa na Hilika wa Zimamoto. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.