Habari za Punde

Mshambuliaji wa Timu ya Zimamoto Hilika Akichuana na Ahmed Katika Ufungaji wa Bao Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora.

 Na: Abubakar Khatib “Kisandu”, Zanzibar.
Mshambuliaji Ahmed Ali Omar wa Jamhuri pamoja na Ibrahim Hamad “Hilika” wa Zimamoto wao ndio vinara wa kupachika mabao kwenye ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora.

Washambuliaji hao mpaka sasa wameshafunga jumla ya mabao 5 kila mmoja katika michezo 8 waliyocheza.
Wanaochuwana na washambuliaji hao ni Mshambuliaji wa Jang’ombe Boys Khamis Mussa “Rais”,Mwalimu Mohd wa Jamhuri pamoja na Abdull Yussuf wa Mwenge ambao wote wameshafunga mabao 4 kila mmoja.
Wengine wanaofuatia ni Seif Saleh wa Okapi, Mussa Ali Mbarouk wa Jamhuri na Hassan Haji wa Zimamoto wote hao wana mabao 3.

Hakim Khamis “Men” ndie Mfungaji bora wa ligi kuu soka ya Zanzibar msimu ulopita alifunga mabao 17 na kuisaidia timu yake Zimamoto kutwaa ubingwa wa ligi hiyo ambapo pia aliwahi kuwa mfungaji bora wa ligi kuu soka ya Zanzibar msimu wa mwaka 2011-2012 wakati Super Falcon ya Pemba ilitwaa ubingwa msimu huo ambapo mpaka sasa hajapewa zawadi yoyote kwa kufanikiwa kuwa mfungaji bora.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.