Habari za Punde

Wasaini wa Sheria Kisiwani Pemba Wapata Elimu ya Sheria Ilioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Tawi la Pemba.

Mkuu wa wilaya ya Chakechake Pemba, Salama Mbarouk Khatib, akifungua mafunzo ya siku moja ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, yaliofanyika na kuandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ tawi la Pemba
Waratibu wa shehia wanaoshughulikia wanawake na watoto wa mkoa wa kusini Pemba, wakifuatilia mada kwenye mafunzo ya kutambulisha kazi za wasaidizi wa sheria, yalioandaliwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ tawi la Pemba
Mratibu wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ‘ZLSC’ tawi la Pemba Fatma Khamis Hemed, akiwasilisha mada, ya dhana ya wasaidizi wa sheria kwa waratibu wa wanawake na watoto wa Mkoa wa kusini Pemba
Afisa Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba Safia Saleh Sultan, akiwasilisha mada ya sheria ya kuwalinda wari na watoto wa mzazi mmoja, kwenye mafunzo kwa waratibu wa wanawake na watoto wa Mkoa wa kusini Pemba, yaliofanyika ZLSC mjini Chakechake
AFISA Mipango wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar ZLSC tawi la Pemba, Khalfan Amour Mohamed, akiwasilisha mada ya sheria ya mtoto  Zanzibar no 6 ya mwaka 2011,  kwa waratibu wa wanawake na watoto wa Mkoa wa kusini Pemba, kwenye mafunzo yaliofanyika ZLSC mjini Chake chake.
(Picha na Haji Nassor, Pemba).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.