Habari za Punde

ZASWA Kufanya Uhakiki wa Wanachama Wake Huku Wakijitayarisha na Uchaguzi. Waandishi wa Michezo Wahimizwa Kujiunga na Chama Hicho.

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Zanzibar (ZASWA) kinatarajia kufanya Uchaguzi wake wa kupata uongozi mpya uchaguzi ambao utafanyika Disemba 24, 2017.

Matayarisho hayo ya Uchaguzi tayari yameshaanza ambapo zoezi linaloendelea sasa ni kuhakiki Wanachama na kutafuta Wanachama wapya ambapo zoezi hilo lilianza tangu July 2, 2017 na litafikia tamati Agost 15, 2017.

Mwinyimvua Abdi Nzukwi ambae ni Mwenyekiti wa Chama hicho amewaomba Waandishi wa Michezo wa Zanzibar kufanya uhakiki kwa wale ambao ni wanachama na kwa Waandishi wapya wanaotaka kujiunga na chama hicho wajitokeze kwa wingi ili wakachukue fomu za kuomba Uanachama.

“Wanachama wetu tunawaomba wajitokezee kuhakiki taarifa zao mana tunaelekea kwenye Uchaguzi mwishoni mwa mwaka, lakini pia nawaomba Waandishi wa michezo wapya waje kuchukua fomu kujiunga na ZASWA watapata fursa nyingi kama ni waandishi wa michezo hapa Zanzibar, waje kuchukua fomu”. Alisisitiza Nzukwi.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.