Habari za Punde

Tamko la Serikali Kuhusu Utaratibu wa Utowaji wa Leseni za Machapisho.

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

BEST 2IDARA YA HABARI-MAELEZO

Simu: +255-22-2126826,
Baruapepe:maelezo@habari.go.tz,
Tovuti: www.tanzania.go.tz,
Faksi: +255-22-2126834.


 
  Mtaa wa Samora,
  S.L.P 8031,
 DAR ES SALAAM.


 
                                              


 


TAARIFA KWA UMMA
KUANZA UTOAJI WA LESENI KWA MAGAZETI NA MAJARIDA
Dar es Salaam, Agosti 23, 2017:

SERIKALI kupitia Idara ya Habari (MAELEZO) inapenda kuutaarifu umma kuwa katika utekelezaji wa matakwa ya kifungu cha 5(e) cha Sheria ya Huduma za Habari, 2016, itaanza kutoa leseni za machapisho mbalimbali ikiwemo magazeti na majarida yote nchini.

Utoaji wa leseni hizo pia ni kwa mujibu wa Kanuni ya 7 ya Kanuni za Sheria ya Huduma za Habari za mwaka 2017 zilizochapishwa kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na 18 la Februari 3, 2017.

Kwa mujibu wa sheria, utaratibu wa sasa unafuta mfumo wa awali wa utoaji wa Hati za Usajili wa magazeti na majarida uliokuwa ukitumika kwa mujibu wa Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 ambayo kwa sasa imefutwa.

Aidha utaratibu huu mpya utawahusu wamiliki wote wa magazeti (newspapers), majarida (journals, magazines na newsletters) na wamiliki wapya ambao hawakuwa wameyasajili machapisho yao. Aidha leseni hizi zitahuishwa kila mwaka kwa mujibu wa Kanuni za 8(3) na 12(1)(2) za Kanuni za Sheria ya Huduma za Habari, 2017.

Fomu za maombi pamoja, akaunti ya kulipia na orodha ya nyaraka zinazohitajika kwa ajili ya usajili vinapatikana kuanzia leo katika ofisi za MAELEZO Dar es Salaam na Dodoma au katika sehemu ya “Huduma Zetu” katika tovuti yetu: www.maelezo.go.tz.

Kwa wamiliki wa magazeti na majarida ambao wana usajili wa zamani, Serikali inatoa fursa  kuanzia leo mpaka Oktoba 15, 2017 wawe wamekamilisha taratibu na kupatiwa leseni mpya za uendeshaji na uchapishaji wa majarida na magazeti na baada ya muda huo hawataruhusiwa kuyachapisha kwani watakuwa wametenda kosa kisheria.
Kwa ufafanuzi zaidi kuhusu utaratibu wa usajili, wasiliana nasi katika namba 0622 664606 na 0717 312417, tembelea tovuti yetu au wasiliana nasi kupitia: maelezo@habari.go.tz
Imetolewa na:
signature2 

Dkt. Hassan Abbasi,

Mkurugenzi Mkuu, Idara ya Habari-MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.