Habari za Punde

Timu ya Taifa ya Jangombe Imebidi Kucheza Mechi Mbili Mfulilizo Kisiwani Pemba Ligi Kuu ya Zanzibar Nane Bora.NJ

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Baada ya kucheza jana Timu ya Taifa ya Jang’ombe na kufanikiwa kuwafunga Jamhuri 2-0 katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar hatua ya 8 bora mchezo uliopigwa kwenye Dimba la Gombani, unaweza kushangaa na leo Taifa wanacheza tena mchezo mwengine wa ligi hiyo hiyo dhidi ya Kizimbani katika uwanja wa Gombani Kisiwani Pemba.

Mchezo huo nambari 48 ulikuwa uchezwe Jumamosi ya Agost 12, 2017 lakini Taifa wameomba wacheze tena na leo ili wawahi kurejea nyumbani Unguja kwaajili ya kupunguza gharama wakiwepo Kisiwani huko.

“Ni kweli Taifa watacheza mechi mbili mfululizo jana na leo kwa vile wameomba wacheze ivyo kwaajili ya kupunguza gharama ili wawahi kurudu nyumbani Unguja kwasababu wakimaliza mchezo huu hawana tena mchezo mwengine hapa Pemba, sasa ukiangalia ratiba mpaka Jumamosi ndo wanacheza na itabidi wasafiri Jumapili gharama zitazidi kuwa kubwa lakini wanacheza leo Alhamis na kesho Ijumaa wanarejea nyumbani”. Kilisema Chanzo.

Ligi kuu soka ya Zanzibar hatua hiyo ya 8 bora inachezwa kwa visiwa viwili tofauti yani Unguja na Pemba ambapo kuna baadhi ya timu ikiwemo Taifa wamesafiri mara mbili tofauti kwenda huko Kisiwani Pemba kucheza michezo yao ambapo mpaka ligi hiyo inaelekea ukingoni hakuna mdhamini yoyote aliyejitokeza jambo ambalo linawapa wakati mgumu vilabu vinavyoshiriki ligi hiyo
Attachments area

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.