Habari za Punde

Ujamaa yalala 3-1 dhidi ya Gulioni katika sherehe za kuadhimisha miaka 60 ya timu ya Ujamaa

Kikosi cha timu ya Gulioni iliyoibuka kifua mbele kwa kuilaza Ujamaa 3-1
Kikosi cha Timu ya Ujamaa iliyolala mbele ya Gulioni


Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Timu kongwe Visiwani Zanzibar Ujamaa Sports Club 

wamekubali kichapo cha mabao 3-1 kutoka kwa vijana wa 

Gulion FC kwenye mchezo maalum wa Sherehe za kutimiza 

miaka 60 kwa Ujamaa mchezo ambao umesukumwa jana 

saa 2 za usiku kwenye uwanja wa Amaan.

Mabao ya Gulioni katika mchezo huo yamefungwa na Abdul Hamid Ramadhan dakika ya 45, Ali Juma dakika ya 71 na Shaabani Hassan dakika ya 88 huku bao pekee la Ujamaa likifungwa na Mwinyi Ame dakika ya 79.

Ujamaa ndio timu aliyewahi kucheza kwa kiwango cha hali ya juu Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein ambapo Katika mchezo huo Mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Habari Utalii Utamaduni na Michezo Zanzibar Mh Rashid Ali Juma akimuwakilisha Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ambae pia alikuwa mlinda mlango hatari wa timu hiyo miaka iliyopita.

Msimu huu mpya wa mwaka 2017-2018 Ujamaa itashiriki ligi daraja la Pili Taifa Unguja wakati Gulioni FC itacheza ligi daraja la Pili Wilaya ya Mjini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.