Habari za Punde

Ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Shein, Kisiwani Pemba Wilaya ya Micheweni.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akisalimiana na  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ZSTC Dkt.Said Seif Mzee mara alipowasili katika  Shamba la Mikarafuu la Kifundi  kwa ajili ya kulikagua shamba hilo na Mikarafuu katika Wilaya Micheweni akiwa katika mwendelezo wa ziara zake katika Mkoa wa Kaskazini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein na Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe.Hamad Rashid Mohamed (katikati) wakifuatana na Viongozi wengine wakati alipotembelea Shamba la Mikarafuu la Kifundi  kwa ajili ya kulikagua shamba hilo na  Mikarafuu katika Wilaya Micheweni akiwa katika mwendelezo wa ziara zake katika Mkoa wa Kaskazini Pemba,(wa pili kulia) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe.Omar Khamis Othman
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akichuma Karafuu katika Shamba la Mikarafuu la Kifundi leo alipokuwa katika mwendelezo wa ziara zake katika Mkoa wa Kaskazini Pemba kwa kulikagua Shamba hilo na kufanya zoezi la Uchumaji,(katikati) Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Mhe.Hamad Rashid Mohamed
Karafuu zilizoanikwa baada ya kuchumwa katika kambi ya karafuu ya Nd,Mohamed Kai Bakar iliyopo katika Kijiji cha Kifundi Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kusini Pemba wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein alipotembelea katika kambi hiyo leo akiwa katika ziara zake katika Mkoa wa Kaskazini Pemba
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Kifundi wakichambua Karafuu katika Kambi ya Nd,Mohamed Kai Bakar iliyopo katika Kijiji cha Kifundi Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kusini Pemba wakati Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein alipotembelea katika kambi hiyo leo akiwa katika ziara zake Mkoa wa Kaskazini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akisalimiana na Nd,Mohamed Kai Bakar Mmiliki wa Kambi ya Karafuu iliyopo katika Kijiji cha Kifundi Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kusini Pemba leo wakati   alipotembelea katika kambi hiyo  akiwa katika ziara zake Mkoa wa Kaskazini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) alipokuwa akitoa nasaha zake kwa Viongozi wa wananchi  baada ya Kuchambua karafuu zilizochumwa katika Kambi ya karafuu ya  Nd,Mohamed Kai Bakari iliyopo katika Kijiji cha Kifundi Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kusini Pemba leo wakati   alipotembelea katika kambi hiyo   akiwa katika ziara zake Mkoa wa Kaskazini Pemba
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akipima karafuu kwa kutumia kipimo cha Pishi na kuzimimina katika Kapu maalum baada ya kuchambua karafuu hizo zilizochumwa katika Kambi ya karafuu ya  Nd,Mohamed Kai Bakari iliyopo katika Kijiji cha Kifundi Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kusini Pemba leo wakati   alipotembelea katika kambi hiyo   akiwa katika ziara zake Mkoa wa Kaskazini Pemba,(kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mhe.Omar Khamis Othman,na (kulia) Waziri asiekuwa na Wizara Maalum Mhe.Sira Ubwa Mamboya, 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi akizungumza na wakulima na wananchi akiwa katika ziara yake Wilayani Micheweni Pemba. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.