Habari za Punde

Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Chakechake akabidhi Ofisi kwa Mkuu wa wilaya mpya

 Alieluwa Mkuu wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Salama Mbarouk Khatib,akimkabidhi taarifa ya Wilaya hiyo, Mkuu wa Wilaya mpya ya Chake Chake  Rashid Hadidi Rashid, ambae ameteuliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Dkt, Ali Mohammed Shein hivi karibuni .

Mkuu wa Wilaya mpya  wa Micheweni Pemba, Salama Mbarouk Khatib, akisaini makabidhiano kwa mkuu wa Wilaya mpya wa Wilaya ya Chake Chake , Rashid Hadidi Rashid, kufuatia mabadiliko ya vituo vya kazi kwa wakuu hao wa Wilaya yaliofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi , Ali Moh'd Shein, hivi karibuni.

 Mkuu wa Wilaya mpya wa Wilaya ya Chake Chake Pemba, Rashid Hadidi Rashid, akizungumza machache kwa watendaji wa Wilaya hiyo baada ya kukabidhiwa dhamana ya kuongoza Wilaya hiyo kutoka kwa mkuu wa Wilaya
anaeondoka  Salama Mbarouk Khatib ambae nakwenda kuendelea na majukumu kama hayo katika Wilaya ya Micheweni Pemba.

 Mkuu wa Wilaya anaeondoka katika Wilaya ya Chake Chake Pemba, Salama Mbarouk Khatib , akizungumza na Masheha , wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama na Watendaji wa Wilaya ya Chake Chake , baada ya kumkabidhi majukumu ya Wilaya hiyo Mkuu wa Wilaya mpya Rashid Hadidi Rashid.

Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya ya Chake Chake Pemba, wakimsikiliza kwa  makini Mkuu wa Wilaya anaeondoka katika Wilaya hiyo, Salama Mbarouk Khatib, akitowa nasaha zake baada ya kumkabidhi Mkuu wa Wilaya mpya Rashid Hadidi Rashid.


Picha na Bakar Mussa -Pemba.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.