Habari za Punde

Jumamosi Kuaza Ligi ya UBA Iliyodhaminiwa na Wamarekani

Na: Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Ligi ya Wilaya ya Mjini (UBA) kwa upande wa Mpira wa Kikapu kwa Wanaume inatarajiwa kuanza rasmi Jumamosi Septemba 9, 2017 katika viwanja vya Gymkhana Mjini Unguja na katika ufunguzi huo siku hiyo kutapigwa mchezo kati ya timu ya POLISI dhidi ya MBUYUNI.

Ligi hiyo imedhaminiwa na kiwanda cha kutengeneza Jezi cha UTA ambacho kipo Marekani wakishirikiana vyema na Chama cha Basketball Wilaya ya Mjini (UBA).

Jumla ya timu 14 zitashiriki ligi hiyo ambazo ni Polisi, Mbuyuni, JKU, Mwembetanga, Cavarias, Stone Town, Africa Magic, Betras, Zan Kwerekwe, Ranger, New West na Nyuki.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.