NA HAJI NASSOR, PEMBA
WAZIRI wa Afya Zanzibar Mhe: Mahamoud Thabiti Kombo,
amewataka watoto wa kike wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba,
wawaripoti watu watakaonza kuwashika shika sehemu zisizostahiki au kuwahonga
kwa vizawadi, kwani huo ndio mwanzo wa wao kubwaka hapo baadae.
Waziri
Mahamaoud alisema, wapo baadhi ya watu wasiowapendelea maendeleo yao, huanza
kuwatambazia mikono kifuani au kuwapa peremendi “pipi” hivyo wanapoona hali
hiyo, wasingojee ushahidi kamili na ni vyema wakaripoti katika maeneo husika.
Akizungumza
katika ufunguzi wa Kituo cha Mkono kwa Mkono “one stop center” kilichopo
hospitali ya Micheweni Mkoani humo, alisema ubakaji huanza na mambo kadhaa
yakiwemo hayo aliyoyataja.
Alisema
wanafunzi na hasa wakike, wasikubali kusubiri ushahidi kamili kwa vile pana
Kituo hicho, bali wajenge utamaduni wa kutoa taarifa kila wanapofanyiwa matendo
yasiowaridhisha.
Waziri
huyo wa Afya, alisema ingawa Kituo hicho kipo, ingawa hawatarajii kuona matendo
ya udhalilishaji ukiwemo ubakaji unaongezeka, bali ni kupunguza na miongoni mwa
njia hizo, ni kutoa taarifa pale wanapoonza kushikwa kifua au kupewa pipi.
“Msikubali
kuchezewa chezewa, au kushikwa shikwa titi zenu au kupewa vipipi na watu mbali
mbali, maana hiyo ndio sababu ya nyinyi wanafunzi na watoto wa kike
kubwa”,alifafanua.
Katika
hatua nyengine Waziri huyo wa Afya Zanzibar Mhe: Mahamoud Thabiti Kombo,
aliwataka wananchi wa Micheweni kushirikiana kwa karibu na watendaji wa Kituo
hicho, ikiwa ni njia moja wapo ya kupunguza matendo ya udhalilishaji wa
kijinsia kwa wanawake na watoto.
Hata
hivyo alisema watendaji wa Kituo hicho pamoja na madaktari wengine, watajengewa
uwezo kwa kupatiwa mafunzo, muda mfupi ujao ili waweze kuwahudumiwa wananchi
kwa ufanisi, kama ilivyo amza ya sirikaki kuu.
Kwa
upande wake Mratibu Mkuu wa masuala ya ulinzi wa uhifadhi wa mtoto kutoka
Shirika la Save Children Zanzibar, Ramadhan Mohamed Rashid, alisema mpango wa
kuanzisha vituo vya aina hiyo, ni mpango maalum wa kuunga mkono juhudi za
serikali kuu.
Alisema,
baada ya wadau mbali mbali wakiwemo na serikali na wizara zake husika, kuona
matendo ya udhalilishaji yanaogezeka siku hadi siku, ndio wakabuni na kuanzisha
vituo hivyo, ili waathirika wahudumiwe.
Hata
hivyo Mratibu huyo, aliwataka madaktari kuacha woga pale wanapotakiwa kufika
mbele ya mahakama kutoa ushahidi wao kwa wale watoto waliowahudumia baada ya
kubakwa, kunajisiwa au kubebeshwa ujauzito.
Akisoma
risala ya wananchi wa Micheweni, daktari wa Hospitali ya wilaya hiyo, Mgeni
Haroun Salim, alisema tokea kuanza kwa huduma za mkono kwa mkono wilayani humo
mwaka 2014, watoto 14 wameshabakwa, nane ujauzito na watoto 12 waliripotiwa kutoroshwa.
Hata
hivyo alisema ujio wa Kituo hicho kipya, sasa kitasaidia kuwafikia wananchi
waliowengi, kwanza kuwahamasisha kukitumia Kituo hicho sambamba na kuwaleleza
athri za matendo hayo ndani ya jamii.
Nae
Mratibu wa Kituo hicho cha Mkono kwa Mkono wilaya ya Micheweni Asma Mohamed
Fasihi, akimpa maelezo Waziri wa Afya mara baada ya kukifungua, alisema
kilichopo mbele yao sasa ni kuwaelimisha wananchi vijijini.
Kituo
cha Mkono kwa mkono kilichomo hospitali ya Micheweni Pemba, ni cha kwanza kati
ya vituo vitano vyengine, vinavyotazamiwa kujengwa na Shirika la Save the
children, ambapo kwa kisiwani Pemba vipo vituo kama hivyo kwa hospitali za Wete
na Chakechake.
No comments:
Post a Comment