Habari za Punde

Charawe yakaribishwa Ligi Kuu, Kilimani City yaanza kwa kishindo
Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.


Timu ya Kilimani City imeanza vyema ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja baada ya kuichapa Kipanga mabao 3-1 katika mchezo uliopigwa saa 8 za mchana katika uwanja wa Amaan.

Mabao ya City yamefungwa na Bakar Bakar Mashango dakika ya 26, Joseph Josephat Kalinga dakika ya 49 na Abdillah Seif Bausi dakika ya 85.

Bao pekee la Kipanga limewekwa nyavuni na Nassor Ali katika dakika ya 90 ya mchezo.

Saa 10 za jioni timu mpya iliyopanda ligi kuu Charawe leo imekaribishwa kwenye ligi hiyo baada ya kuchapwa bao 1-0 na KVZ.
 
Bao pekee la KVZ limefungwa na Rafael Mwambeleko dakika ya 65 ya mchezo huo.


Ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja itaendelea tena kesho kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan.

Saa 10 za jioni wataanza kati ya Maafande wa Polisi kwa kucheza na Miembeni City, na saa 1 za usiku watakipiga Taifa ya Jang’ombe dhidi ya Zimamoto.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.