MWENYEKITI wa Kamati ya GEWE III, Sheha wa shehia ya Mjini
Ole, Khamis Shaaban (katikati), akifungua mkutano wa kuwaelimishwa wanakamati
hiyo, aina za kesi za udhalilishaji, mkutano uliofanyika uwanja wa Gombani
Chakechake Pemba
MRATIBU wa
miradi kutoka TAMWA Asha Abdi Makame, akielezea ujio wa mradi wa kupinga
udhalilishaji GEWE III, kwa ajili ya shehia sita za Wiaya ya Wete kisiwani
Pemba, mkutano huo ulifanyika uwanja wa Gombani
MWANASHERIA wa serikali kutoka Afisi ya Mkurugenzi wa
Mashitaka Pemba, Mohamed Ali Juma akitoa mada ya aina ya makosa ya
udhalilishaji, mbele ya kamati ya mradi wa kupinga udhalilishaji kupitia GEWE III, uliofanyika
uwanja wa Gombani
AFISA Ustawi
wa Jamii wilaya ya Wete Haroub Suleiman Hemed, akichangia jambo, kwenye mkutano
uliojadili aina ya makosa ya udhalilishaji, kupitia mradi wa kupinga
udhalilishaji GEWE III, na kufanyika uwanja wa Gombani Chakechake Pemba
Mwanakamati wa Mradi wa GEWE III, akichangia wakati wa mkutano huo wa siku moja, uliozungumzia aina ya makosa ya udhalilishaji, uliofanyika uwanja wa
Gombani Chakechake Pemba, ambapo mradi huo uko kwenye shehia za Mchanga mdogo,
Kinyikani, Kiungoni, Mjini ole, Kangagani na Shengejuu.
WANAKAMATI ya mradi wa GEWE III, waliohudhuria mkutano wa
siku moja, uliozungumzia aina ya makosa ya udhalilishaji, uliofanyika uwanja wa
Gombani Chakechake Pemba, ambapo mradi huo uko kwenye shehia za Mchanga mdogo,
Kinyikani, Kiungoni, Mjini ole, Kangagani na Shengejuu, (Picha na Haji Nassor, Pemba).
No comments:
Post a Comment