Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja imeendelea tena
leo kwa kupigwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan
ambapo saa 8 za mchana Zimamoto na Kipanga zilishindwa
kutambiana baada ya kutoka sare ya kufungana bao 1-1.
Bao la Kipanga limefungwa na Nassor Ali wakati bao la Zimamoto likiwekwa nyavuni na Hassan Haji.
Saa 10 za jioni katika uwanja huo KVZ wakaitandika Polisi bao 1-0 kwa lililofungwa na Salum Songoro dakika ya 79.
Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa mchezo mmoja katika uwanja wa Amaan saa 10:00 za jioni kati ya Jang’ombe boys dhidi ya Chuoni.
No comments:
Post a Comment