Habari za Punde

Chinonso apiga Hat trick baada ya Chuopni kuichakaza Charawe 4-0

Mshambuliaji wa Timu ya Chuoni , Charles Chinonso akikabidhiwa mpira na Abdallah Thabit, Mjumbe wa ZFA Taifa baada ya kuisaidia timu yake ya Chuoni kuondoka na ushindi wa 4-0 wakati yeye mwenyewe akipiga matau

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Mshambuliaji Charles Chinonso amefunga mabao matatu (Hat-trick) na kuiongoza Chuoni kuichakaza Charawe kwa mabao 4-0 kwenye mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar Kanda ya Unguja uliopigwa jioni ya leo kwenye uwanja wa Amaan.

Chinonso amefunga mabao hayo katika dakika ya 9, 11 na 26 huku bao jengine likifungwa na Mustafa Zakaria dakika ya 49.


Mapema saa 8 za mchana timu ya Miembeni City ikaendelea rikodi yake mbovu ya kufungwa baada ya leo kufungwa 2-1 na Kipanga.

Mabao ya Kipanga yamefungwa na Imran Abdul dakika ya 8 na Said Salum dakika ya 32 na lile la Miembeni City limefungwa na Feisal Riambi dakika ya 18.

Ligi hiyo itaendelea tena kesho kwa kupigwa mchezo mmoja katika uwanja wa Amaan majira ya saa 10:00 za jioni kati ya Taifa ya Jang'ombe dhidi ya KVZ.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.