Habari za Punde

Kamara awapongeza waamuzi kutoka Zanzibar waliopata Beji ya FIFA

Katibu wa waamuzi wa Soka Zanzibar Muhsin Ali 'Kamara'

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Katibu wa Waamuzi wa Soka Zanzibar Muhsin Ali “Kamara” amewapongeza waamuzi wanne wa Zanzibar waliyopata beji ya FIFA.

Kamara amesema ni faraja kwa Zanzibar kutoa waamuzi wa nne wenye beji hiyo ya FIFA.

Juzi Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA), limetoa beji kwa Waamuzi 18 wa Tanzania kati yao wane kutoka Zanzibar katika msimu wa mshindano mwaka 2018.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka FIFA, Waamuzi walioteuliwa kutoka Zanzibar ni Mfaume Ali akiwa ni Muamuzi wa kati huku Wasaidizi walipewa beji hizo Mgaza Kunduli, Mbaraka Haule na mwanamama Dalila Jaffari.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.