Habari za Punde

Kamati ya Biashara Kilimo na Fedha ya Baraza la Wawakilishi Yatembelea Mradi wa Ujenzi wa Maduka ya Kisasa Katika Jumba la Treni Darajani Zanzibar.

Ujenzi wa Jengo la Nyumba ya Treni Darajani ukiendelea na ujenzi wake wa maduka ya kisasa katika eneo hilo unaofanywa na Kampuni ya Ujenzi ya Kichina ya CRJE ukiwa katika hatua za kukamilika kwa ujenzi huo na kutowa fursa kwa Wananchi na Wafanya biashara kutowa huduma.
 Mradi huu wa Ujenzi unaosimamiwa na Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF.     
Kaimu Meneja Mipango na Uwekezaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) Abdulazizi Ibrahim Iddi akitowa maelezo ya Mradi huo wa maduka ya kisasa katika jengo la Treni Daraji wakati wa Kamati hiyo kutembelea mradi huo kujionea maendeleo yake. Kamati hiyo inaongozwa na Mwenyekiti wake Mhe Yussuf Hassan Iddi akifunga mikono katikati. 
Mkurugenzi Muendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF, Bi Sabra Issa Machano akitowa maelezo kwa Wajumbe wa Kamati ya Biashara Kilimo na Fedha ya Baraza la Wawakilishi wakati ilipotembelea Mradi wa Ujenzi wa Maduka ya Kisasa katika Jumba la Treni Darajani Zanzibar. 
Kaimu Meneja Mipango na Uwezeshaji Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF Abdulazizi Ibrahim Iddi akitowa maelezo ya ujenzi huo.
Wajumbe wakifuatilia maelezo wakati wa ziara yake kutembelea Mradi wa Ujenzi wa Jumba la Treni Darajani.
Mjumbe wa Kamati ya Biashara, Kilimo na Fedha Mhe Ussi Khamis akiuliza swali kwa wahusiika na Mradi huo wa Ujenzi wakati wa ziara yao katika eneo la ujenzi. 
Sehemu ya maduka katika jumba la Treni Darajani likiendelea na ujenzi wake.
Mafundi wakiendelea na Ujenzi huo katika jengo hilo la Darajani Zanzibar.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar ZSSF Sabra Issa Machano akiagana na Wajumbe wa Kamati baada ya kumaliza ziara yao kutembelea Mradi huo wa Jumba la Treni Darajani. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.