Habari za Punde

Khamis Mussa (Rais) apiga Hat-trick Boya ikiichapa Charawe 4-2


Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Mshambuliaji wa timu ya Jang'ombe Boys Khamis Mussa (Rais) amefanikiwa kuondoka na mpira uwanjani baada ya kufunga mabao 3  yani Hat trick.

Amefunga mabao hayo wakati Boys walipoipiga Charawe mabao 4-2 katika mchezo wa ligi kuu soka ya Zanzibar kanda ya Unguja uliosukumwa mchana wa leo katika Uwanja wa Amaan.

Rais amefunga mabao hayo katika dakika ya 3, 9, na 21  na bao la nne likifungwa na Hafidh Bariki (Fii) dakika ya 83 huku mabao ya Charawe yakiwekwa nyavuni na Ulimwengu Edimundi dakika ya 66 na Yussuf Mkubwa dakika ya 68.

Mara baada ya kumalizika mchezo huo Mtandao huu umefanikiwa kuzungumza na mchezaji huyo huku akipania kuongoza kwa kufunga mabao katika ligi hiyo.

“Nimefurahi sana kufunga mabao 3, niliwahi kufunga hat trick mwaka jana, ila mwaka huu nataka kuchukua ufungaji bora". Alisema Rais.

Hii ni Hat-trick ya pili kufungwa katika ligi hiyo ndani ya msimu huu ambapo Hat-trick ya kwanza ilifungwa na Salum Songoro wa KVZ ambapo mpaka sasa wanaongoza kwa mabao katika ligi hiyo ni washambuliaji hao pamoja na Nassor Ali wa Kipanga wote wakiwa na mabao 4.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.