Habari za Punde

Kikosi cha Zanzibar Heroes na Zanzibar Queens kutangazwa leo


Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kocha Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) , Hemed Suleiman (Morocco)  leo Jumapili Novemba 5, 2017 saa 10:00 za jioni atatangaza majina ya wachezaji watakaounda kikosi hicho. 

Zanzibar Heroes, inajiandaa kushiriki Mashindano ya Chalenj Cup ambayo yanaandaliwa na CECAFA kwa kushirikisha nchi za Afrika Mashariki na Kati na mwaka huu yatafanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 25 huku nchi zinazotarajiwa kushiriki ni Kenya, Uganda, Tanzania Bara, Rwanda, Burundi, Sudan, Ethiopia, Sudan ya Kusini, Djibout, Elitrea, Somalia na Zanzibar huku Zimbabwe na Libya zimealikwa kama wageni kushiriki.

Mbali ya kutangaza kikosi hicho pia kocha Morocco kesho anatarajiwa kutangaza majina ya wachezaji wa timu ya Taifa ya Zanzibar ya Wanawake "Zanzibar Queens ambayo inatarajiwa kwenda nchini Rwanda kushiriki mashindano ya CECAFA ya wanawake.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.