Habari za Punde

Kocha Salahi kateuliwa kuwa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar ya wanawake

Kocha Mohammed Ali Salahi (Richkard)

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes), Hemed Suleiman (Morocco) amemteuwa kocha Mohammed Ali Salahi (Richkard) kuwa kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar ya Wanawake (Zanzibar Queens).

Uteuzi huo umefanyika leo Jumanne ambapo kocha Salahi atafundisha kikosi hicho kitakachokwenda nchini Rwanda kwenye Mashindano ya CECAFA Woman Chalenj CUP yanayotarajiwa kufanyika muda wowote mwezi huu.

Baada ya uteuzi huo tumemtafuta kocha huyo akizungumzia uteuzi wake ambapo amefurahishwa sana huku akiwaahidi Wazanzibar kufanya makubwa katika kikosi hicho.

Jana Kikosi hicho kilitangazwa na kilikuwa hivi.

WALINDA MLANGO

Salma Abdallah (Green Queens)
Hajra Abdallah (Jumbi)
Mtumwa (New Generation Queens)

WALINZI 

Hawa Ali (New Generation Queens)
Mtumwa Khatib (Women Fighter)
Aziza Mwadini (New Generation Queens)
Flora Kayanda (Jumbi)
Safaa Makirikiri (New Generation Queens)
Neema Suleiman (Jumbi)

VIUNGO

Mwajuma Ali (Jumbi)
Nasrin Mohd (Women Fighter)
Riziki Abdallah "Chadole" (Jumbi)
Aziza Ali (Jumbi)
Sijali Abdallah (Green Queens)

WASHAMBULIAJI 

Mwajuma Abdallah (New Generation Queens)
Shadida Abdallah (Women Fighter)
Neema Machano (Jumbi)
Dawa Haji (Women Fighter)
Sabah Hashim "Mess" (New Generation Queens)
Greece Ronald (Green Queens)

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.