Habari za Punde

Yaliosemwa na Dk.Hassan Abbas Katika Kipindi Cha Vijana Tz Juu ya Mafanikio / Utendaji wa Serikali na Changamoto Katika Tasnia ya Habari.

"Ofisi yangu ina jukumu la kutoa taarifa sahihi na kwa wakati ya Serikali; Kusajili na kufungua Magazeti; Kusaidia Watu wa mifumo mingine ya Serikali kusema" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Uhuru wa vyombo vya habari upo wa kutosha. Serikali imeruhusu uhuru wa Vyombo vya habari. Kuna Redio zaidi ya 150, tuna redio zaidi ya 30, kuna Magazeti zaidi ya 110 yanayotoka nchini" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Serikali ina simamia Wananchi wapate habari sahihi na si kulishwa habari mbovu. Serikali tunalisimamia hili" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Changamoto iliyopo ni kuhakikisha habari zsahihi zinawafikia Watu wote kwa wakati" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Rais @MagufuliJP amefanikiwa sana kuleta mageuzi ya kifikra. Kujenga hari ya Uzalendo, nidhamu, uwajibikaji kwa Watu wake wakiwemo Watumishi wa Umma na Wananchi" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Rais @MagufuliJP ameleta nidhamu kubwa ya matumizi ya fedha za umma. Mathalani amefanikiwa kudhibiti safari za nje zisizo na tija" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Hapo nyuma zilitumika bilioni zaidi ya 200 kwa safari tu wakati hivi sasa zimetumika bilioni 25 tu kwa safari tumeokoa pesa nyingi"@TZ_MsemajiMkuu
"Rais @MagufuliJP ameleta mageuzi ya kudhibiti Wafanyakazi hewa zaidi ya 20,000 na kuokoa zaidi ya Tsh. Bilioni 238. Ni mageuzi makubwa" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Tumeondoa wafanyakazi hewa takribani elfu 20 kwa zoezi hilo tumeokoa bilioni 238" @TZ_MsemajiMkuu
"Hawa wanaopiga kelele juu ya mageuzi ya rasilimali za madini. Ipo siku watanyamaza wakiona manufaa ya wazi. Serikali ya @MagufuliJP imeonyesha uzalendo kwenye madini" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Zipo nchi kubwa duniani awapati 50/50 kwenye Madini sisi tumeweza @TZ_MsemajiMkuu
"Serikali itaendelea kuhakikisha kila kilicho chetu tunakipata"@TZ_MsemajiMkuu
"Kwenye vyeti feki Serikali ya Rais @MagufuliJP imeokoa zaidi ya Tsh. Bilioni 148 ambazo zinaenda kwenye shughuli za kimaendeleo." - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Sekta ya habari ni sekta nyeti na Sheria hii ya habari tuliyo nayo sasa imeleta maboresho na ubora kwenye sekta ya habari nchini" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Huwezi kutoa habari kwa kuingilia faragha ya mtu" @TZ_MsemajiMkuu
"Huwezi ukakiacha kituo cha radio kinawachochea wakulima wakawaue wafugaji arafu ukasema wana haki ya habari "@TZ_MsemajiMkuu
"Sheria mpya ya huduma ya habari vimeweka ustawi wa vyombo vya habari na si kweli ipo kwa ajili ya kufungia habari." - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Popote duniani hakuna nchi yenye sheria inayosema andika chochote" @TZ_MsemajiMkuu
"Hakuna nchi yeyote Duniani inayotoa Uhuru kwa vyombo vyao vya habari kuwa na uhuru wa kuandika chochote kile wanachojisikia" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Uandishi wa habari ni taaluma sasa ukikiuka sisi kama serikali hatuwezi kukuacha"@TZ_MsemajiMkuu
"Sisi tunailea sekta yote ya habari"@TZ_MsemajiMkuu
"Wananchi wapuuze habari kuwa Serikali inafungia vyombo vya habari inapojisikia bali ina zingatia sheria" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Chombo cha habari kinatakiwa kifuate miiko"@TZ_MsemajiMkuu
"Vijana waamue kufanya kazi, wawe Wazalendo, wamwogope Mungu. Safari ya Mabadiliko ni ngumu lakini inahitaji uvumilivu" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Watanzania wamuunge mkono Rais @MagufuliJP atimize utekelezaji wa ilani ya uchaguzi" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Mwakani 2018 mwezi Julai Serikali italeta ndege kubwa ya kisasa itakayokuwa inakwenda popote pale Duniani" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
Mheshimiwa Rais @MagufuliJP alikuta mikopo inatolewa kiasi cha bilioni 48 kwa mwaka Lakini sasa hivi tumefikia bilioni 472 @TZ_MsemajiMkuu
"Fedha zipo na watapata kila mwanafunzi mwenye haki ya kupata"@TZ_MsemajiMkuu
"Serikali ya Rais @MagufuliJP inatoa Tsh. Bilioni zaidi ya 400 kwa Wanafunzi. Kwa mara ya kwanza fedha imetangulia vyuoni kabla ya Wanafunzi kuanza masomo" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Serikali imeboresha makusanyo kutoka Tsh. Trilioni 9.9 mpaka Tsh. Trilioni 14 kwa mwaka" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
Mheshimiwa @MagufuliJP alipoingia madarakani tulikuwa tunakusanya kodi kwa kiasi cha "Trilioni 9.9.Leo hii tunakusanya trilioni 14 kwa mwaka haya ni mafanikio makubwa"@TZ_MsemajiMkuu
"Serikali imeleta miradi ya kihistoria nchini ya kuzalisha umeme kupitia miradi ya Kinyerezi 1 & 2" - Dk. H.A @TZ_MsemajiMkuu
"Hivi tunapozungumza kuna watu hawalali kuna watu wanajenga reli Usiku na mchana"@TZ_MsemajiMkuu
Dk. Hassan Abbas ni Mkurugenzi Mkuu Idara ya Habari na Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali aliyasema hayo katika kipindi cha VijanaTz kilichorushwa Mubashara siku ya Ijumaa Novemba 10, 2017 kupitia mitandao ya kijamii ya UVCCM ya Twitter, Facebook na Instagram
IMEANDALIWA NA;
Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi
UVCCM Taifa

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.