Habari za Punde

Balozi Seif ashiriki usafi wa mazingira hospitali ya Chake Chake ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar


 MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Idd, akishiriki katika usafi wa mazingira katika hospitali ya Chake Chake, Pamoja na viongozi mbali mbali wa serikali akiwemo mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba, Hemed Suleiman Abdalla, katibu tawala mkoa huo Yussuf Mohamed Ali na Kamanda wa Polisi Mkoa kusini Sheikhan Mohamed Sheikhan, ikiwa ni uzinduzi wa shamrashamra za kuadhimisha miaka 54 ya Mpainduzi matukufu ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)


 MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akitoka katika Hospitali ya Chake Chake, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla, mara baada ya kumaliza usafi wa mazingira ikiwa ni uzinduzi wa shamrashamra za kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)


 KATIBU Tawala Mkoa wa Kaskazini Pemba, Yussuf Mohamed Ali akizungumza na wananchi mbali mbali wa chake chake, wakati wa uzinduzi wa shamrashamra za kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)MKUU wa Mkoa wa Kusini Pemba Hemed Suleiman Abdalla akitoa salamu za wananchi wa mkoa huo, kwa makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, wakati wa uzinduzi wa shamrashamra za kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliyofanyika katika kiwanja cha Tenisi Chake Chake.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)


 MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe:Balozi Seif Ali Iddi, akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Chake Chake katika uwanja wa Tenisi, baada ya kumalizika kwa zoezi la usafi katika hospitali ya Chake Chake, ikiwa ni uzinduzi wa shamarashama za kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA) WANANCHI mbali mbali wa mji wa Chake Chake wakisikiliza kwa makini hutaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, wakati alipokuwa akizungumzanao baada ya kuzindua shamrashamra za kuadhimisha miaka 54 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA)
BAADHI ya wafanyakazi wa Wizara ya Habari Utalii utamaduni na Michezo Pemba, wakifanya usafi katika jengo la Wizara hiyo, ikiwa ni uzinduzi wa shamrashamra za miaka 54 ya Mapinduzi ya matukufu ya zanzibar.(PICHA NA ABDI SULEIMAN,PEMBA).

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.