Habari za Punde

Ofisi ya Makamu wa Rais Yakanusha Tangazo Linalotangaza Ushiriki wa Makamu wa Rais Kupanda Miti Tarehe 1, January 2018.

TAARIFA KWA UMMA
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakanusha tangazo linalosambaa katika Mitandao ya Kijamii linalomhusisha Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan  kuwa atashiriki zoezi la kupanda miti kwenye Chuo Kikuu Cha Dodoma siku ya tarehe 1-1-2018. Ofisi ya Makamu wa Rais inapenda kuujulisha umma kuwa tangazo hilo si la kweli na Makamu wa Rais hana ratiba ya kupanda miti kwenye chuo hicho kwa tarehe iliyotajwa.

Ikumbukwe kuwa siku ya tarehe 15-12-2017 wakati wa hafla ya kuhamia Makao Makuu ya Nchi, Makamu wa Rais wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan alitangaza kampeni ya kupanda miti Dodoma ambayo itaratibiwa na Ofisi yake .

Ofisi ya Makamu wa Rais inawataka Wananchi kuzingatia matangazo, taarifa na ratiba zitakazotolewa na Ofisi yake kuhusu programu ya upandaji miti Dodoma.

Imetolewa na:
Ofisi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dodoma

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.