Habari za Punde

Waziri Haji Omar Kheir azindua Wodi ya wazazi ya kinamama ikiwa ni mwendelezo wa shamra shamra za miaka 54 ya mapinduzi

Na Ali Issa Maelezo   3/1/2018 

Waziri wa nchi afisi ya Rais Tawala za mikoa na idara maalum za Serikali Haji Omar Kheir amewataka kinamama kujifungulia Hospitalini na kuacha mazoea ya kujifungulia nyumbani ili kuepuka matatizo yanayoweza kujitokeza. 

Hayo ameyasema leo katika kituo cha Afya cha Sebleni wakati wa uzinduzi wa Wodi ya wazazi ya kinamama wa zaidi ya shehia saba ikiwa ni mwendelezo wa shamra shamra za miaka 54 ya mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema kinamama kujifungulia hospitali kuna wapa asilimia kubwa kuzaa salama kwani inapotokea tatizo inakuwa ni rahisi kulitatua,kuliko kujifungulia nyumbani.

Amesema frusa hiyo waitumie na waache kwenda jifungulia nyumbani kwani vituo vya Afya vipo kwa ajiliyao navinatoa huduma bure kwa kuzaa.

“Nakuombeni acheni kujifungulia nyumbani kwa sababu nyumbani hakuna utalamu wa kutosha na likitokea tatizo ni vigumu kulikabili”alisema Waziri huyo.

Waziri huyo akijibu changamoto ya kutoajiriwa wafanyakazi wanao jitotea waliopo hapo waliokuwa hawajaajiriwa kwa kipindikirefu ameitaka Ofisi ya mkoa, wilaya na manispaa kulitatua tatizo hilo kwa kulifikisha idara ya uajiri ili ufumbuzi wa ajira upatikane.

Nae mkuu wa mkoa wa mjini magharibi Ayoub Mohammed Mahmoud amesema kuwa kufunguliwa kwa wodi hiyo ni fursa ya kipekee kwa mkoa huo una idadi kubwa ya wazazi wanao kwenda hospital ya mnazi mmoja hospitali kujifungua.

Amesema malengo na dhamira ya mapinduzi ya Zanzibar ni kuwaondolea wananchi matatizo yanayo husiana na huduma za kijamii ikiwemo Afya,maji,elimu hivyo ni jukumu la wananchi kuzidisha mashirkiano kwa serikali yao.  

Nae Mkurugenzi Mkuu Wizara ya Afya Dkt. Jamala Adam Taib alisema ujenzi wa wodi hiyo ni msaada wa Shirika la DANIDA na UNFPA kujenga ukuta na kutoa vifaa tiba.

Wodi hiyo ya Wazazi kwa sasa itakuwa inazihudumia shehia saba ikiwemo Sebleni, Amani,kilimahewa,magogoni, na Kwa mtipura.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.