Habari za Punde

Waziri Kheir azindua kituo cha usindikaji mazao Pujini Pemba, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Joseph Abdalla Meza akitoa taarifa ya Kitaalamu juu ya ujenzi wa kituo cha usindikaji mazao kilichopo Pujini Wilaya ya Chake Chake ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar.
 Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Pemba, Hemed Suleiman Abdalla, akitowa waadhi wake kwa Wananchi waliohudhuria katika hafla ya ufunguzi wa kituo cha usindikaji mazao huko katika kituo cha Pujini Pemba, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar.
 Naibu waziri wizara ya Kilimo , Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya  Mapinduzi Zanzibar, Lulu  Msham Khamis,akitowa maelezo juu ya ujenzi wa kituo cha usindikaji mazao huko Pujini, kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara maalumu za SMZ, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar.
Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za mitaa na Idara maalum za SMZ, Haji Omar Kheir, akizungumza na Wananchi mbali mbali waliohudhuria katika ufunguzi wa kituo cha usindikaji mazao ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za miaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar.

 Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Idara maalumu za SMZ, Haji Omar Kheir, akiangalia ramani ya jengo la kituo cha usindikaji wa mazao huko katika kijiji cha Pujini Pemba,
Picha ya kituo cha usindikaji matunda kilichofunguliwa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa , Serikali za mitaa na Idara maalumu za SMZ, Haji Omar Kheir , huko Pujini Pemba, ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za kiaka 54 ya Mapinduzi Zanzibar.

PICHA NA SAID ABDULRAHAMAN - -PEMBA.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.