Habari za Punde

Wafanyakazi wa Mgodi wa Bulyanhulu Wafanya Sherehe za Kuukaribisha Mwaka Mpya 2018 'SIKUKUU YA FAMILIA'

WAFANYAKAZI WA MGODI WA BULYANHULU WAFANYA SHEREHE KUKARIBISHA MWAKA MPYA 2018 'SIKUKUU YA FAMILIA'

Wafanyakazi wa mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga pamoja na familia zao wamesherehekea Sikukuu ya Familia ‘Acacia Bulyanhulu Family Day 2018’ kwa ajili ya kuuaga mwaka 2017 na kuukaribisha mwaka 2018.

Sikukuu hiyo imefanyika Jumamosi Januari 6,2018 katika uwanja wa michezo wa mgodi wa Bulyanhulu uliopo kata ya Kakola halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na wafanyakazi wa mgodi huo na familia zao ambapo mgeni rasmi alikuwa mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu.
Akizungumza wakati wa kusherehekea sikukuu hiyo,Meneja wa migodi ya Bulyahulu na Buzwagi,Benedict Busunzu alisema lengo la sikukuu hiyo ni wafanyakazi na familia zao kujumuika pamoja kufurahia mwisho wa mwaka uliopita na kujitayarisha kwa ajili ya mwaka mpya 2018.
“Katika kusherekea sikukuu hii  tumeialika jamii inayotuzunguka kujumuika nasi kwa ajili ya kuonesha upendo,tunaonesha pia shughuli tunazofanya,vikundi vya wajasiriamali vinavyozunguka mgodi ambao tumekuwa tuvikiviwezesha kutengeneza bidhaa mbalimbali ambavyo vitakuwa na ushindani mkubwa katika masoko,tuna imani mwaka huu utakuwa na mafanikio makubwa”,alieleza Busunzu.
Busunzu alisema hivi sasa mgodi umeanza shughuli za uzalishaji lakini uzalishaji umepungua kutokana na matatizo yaliyojitokeza mwaka 2017 na kuongeza kuwa wataendelea kutekeleza miradi waliyokuwa wameahidi kuifanya.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu aliupongeza mgodi huo kwa kuendelea na utamaduni wa kuandaa sikukuu ya familia kwani wamekuwa wakiwakutanisha wafanyakazi wa mgodi na jamii inayowazunguka.
“Shughuli hizi za kukutanisha watu pamoja zinajenga jamii,nimekuwa nikihudhuria sikukuu hizi,mwaka jana nilihudhuria pia sikukuu ya familia katika mgodi wa Buzwagi,na hakuna tatizo lolote linalotokea,niwapongeze sana kwa kuunganisha jamii”,alieleza Nkurlu.
Katika kusherehekea sikukuu hiyo,mbali na washiriki  kula,kupata vinywaji,kucheza pia shughuli mbalimbali zimefanyika ikiwemo maonesho ya mitambo inayotumika kuchimbia madini katika mgodi huo,maonesho ya vikundi vya wajasiriamali wanaozunguka mgodi huo,utoaji damu,utoaji wa zawadi kwa watoto na burudani mbalimbali zikiongozwa na kundi la sanaa la Mrisho Mpoto 'Mjomba team'.
Uongozi wa mgodi huo,pia umetumia fursa hiyo kukabidhi mabati 64 na matofali zaidi ya 2900 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Beya iliyopo katika halmashauri ya Nyang’hwale mkoani Geita ambayo hivi karibuni majengo yake yalibomoka baada ya mvua kubwa kunyesha. ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Meneja wa migodi ya Bulyahulu na Buzwagi,Benedict Busunzu akielezea lengo la Sikukuu ya Familia ‘Acacia Bulyanhulu Family Day 2018’ Jumamosi Januari 6,2018 katika uwanja wa michezo wa mgodi huo-Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog 
Wajumbe wa kamati ya maandalizi ya Sikukuu ya Familia mgodi wa Bulyanhulu mwaka 2018 ‘Acacia Bulyanhulu Family Day 2018’wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kutambulishana
Mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu akizungumza wakati wa Sikukuu ya Familia ‘Acacia Bulyanhulu Family Day 2018’
Keki maalumu kwa ajili ya Sikukuu ya Familia ya Bulyanhulu
Mrisho Mpoto 'Mjomba' aliyekuwa MC mkuu katika sikukuu ya Familia ya Bulyanhulu mwaka 2018 akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu ili aimbe live wakati wa sikukuu hiyo
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu akiongoza Live Band ya Mrisho Mpoto 'Mjomba'.Mkuu huyo wa wilaya ambaye ni mlezi wa Mrisho Mpoto Live Band alionesha umahiri wake wa kuimba nyimbo mbalimbali ukiwemo wa Mario
Mfanyakazi wa mgodi wa Bulyanhulu akicheza na mtoto wake
Burudani inaendelea
Kulia ni Meneja wa migodi ya Bulyahulu na Buzwagi,Benedict Busunzu (kulia) akionesha uwezo wake wa kucheza
Michezo ya watoto ikiendelea wakati wa sikukuu ya familia
Mrisho Mpoto akiimba na kucheza na watoto
Watoto wakicheza muziki
Mchekeshaji Oscar Nyerere akiwa na Mrisho Mpoto wakati akiigiza sauti ya rais John Pombe Magufuli
Hatari sana....Vijana kutoka kundi la sanaa la Mrisho Mpoto wakitoa burudani
Tunafuatilia matukio yanayoendelea...
Chakula nacho kilikuwepo cha kutosha,pichani ni foleni kuchukua chakula 
Nyama choma nazo zilikuwepo
Burudani kutoka Kundi la Mjomba Mpoto ikiendelea..
Zoezi la utoaji zawadi ya vifaa vya shule kwa watoto likiendelea
Zoezi la utoaji damu kwa hiari likiendelea....
Muda wa kutembelea Vibanda vya wajasiriamali wanaoishi karibu na mgodi ambao wanawezeshwa na mgodi huo wa Bulyanhulu: Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu akiangalia CD kuhusu ufugaji kuku wa mayai ya kienyeji katika banda la kikundi cha ufugaji kuku cha Mamuu Chicken. 
Kushoto ni Mzee Samwel Igoko akimwelezea Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu kuhusu mradi wao wa ufugaji wa nyuki na kumuonesha asali waliyotengeneza
Mkuu wa wilaya ya Kahama,Fadhili Nkurlu akiangalia mitambo inayotumika kuchimba madini ya dhahabu katika mgodi wa Bulyanhulu..Pichani ni mtambo unaotumika kama ngazi kufanyia kazi za juu
Meneja wa migodi ya Bulyahulu na Buzwagi,Benedict Busunzu akimkabidhi kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Nyang'hwale Rajabu Mmunda bati moja kati ya mabati 64 yaliyotolewa na mgodi huo kusaidia ujenzi wa shule ya msingi Beya ambayo majengo yake yalibomolewa na mvua kubwa iliyonyesha hivi karibuni
Kushoto ni Meneja wa migodi ya Bulyahulu na Buzwagi,Benedict Busunzu akimkabidhi kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Nyang'hwale Rajabu Mmunda tofali kati ya matofali zaidi ya 2900 yaliyotolewa na mgodi huo kusaidia ujenzi wa shule ya msingi Beya iliyopo katika halmashauri ya Nyang'hwale
Mfanyakazi wa Bulyanhulu bwana Terry Little akiwa amebeba nyoka na watalaamu kwa kucheza na nyoka kutoka kundi la Mrisho Mpoto
Mfanyakazi wa Bulyanhulu akiwa amebeba nyoka...
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog ANGALIA PICHA NYINGI ZAIDI <<HAPA>>

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.