Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Mmanga Mjengo Mjawiri akizungumza na Walimu, Wanafunzi na Kamati ya Wazee Skuli ya Chokocho katika Ziara Maalumu ya kuzitembelea Skuli zilizofanya vibaya katika matokeo ya mitihani ya Taifa. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafuzo ya Amali Zanzibar Mh. Abdalla Mzee na Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Mkoani Mh. Issa Juma Ali
Walimu, wanafunzi Wajumbe wa kamati ya Wazee Skuli ya Chokocho na wadau mbali mbali wa Elimu kisiwani Pemba katika ziara maalumu ya Mh. Naibu waziri wa Elimu Mh. Mmaga Mjengo Mjawiri Skuli ya Chokocho.
Na
Ali Othman, Pemba
Naibu
waziri wa Elimu na Mafunzo ya amali Zanzibar Mh. Mmanga Mjengo Mjawiri amefanya
ziara maalumu kisiwani Pemba ya kuzitembelea Skuli zilizofanya vibaya katika
mitihani ya Taifa mwaka 2017.
Mh.
Mmanga ameanza ziara hiyo Skuli ya Chokocho wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini
Pemba ambayo nimiongoni mwa Skuli tano za mwisho kwamatokeo mabaya ya mtihani
wa kidato cha nne mwaka 2017.
Akionesha
kutoridhishwa na matokeo hayo alipokutana na kamati ya wazee, walimu na
wanafunzi wa skuli ya Chokocho katika ukumbi wa sSkuli hiyo, Mh. Mmanga amesema
hali hiyo inasikitisha na Serikali haipendi kuona skuli zake zikifanya vibaya
hasa kwa vile miundo mbinu kama vile maabara ipo.
Akipitia
sababu mbali mbali zilizotajwa kua chanzo cha matokeo hayo mabaya kwa baadhi ya
skuli alizowahi kutembelea kisiwani Unguja Mh. Mmanga amesema, kwa baadhi ya
skuli sababu zilizotajwa ni utoro wa
wanafunzi na kutokujali masomo yao, ushiriki mdogo wa wazazi, mabadiliko ya
mitaala na uhaba wa vifaa.
Hata
hivyo Mh, Mmanga amesema katika ufundishaji mtu muhimu sana ni mwalimu hivyo
amewataka walimu kufundisha kwa viwango bora, kupima kwa viwango sahihi na
kutoa mrejesho kwa wakati.
Mh.
Mmanga ameonya tabia ya baadhi ya walimu kutumika katika Skuli binafsi na
kuacha kutekeleza ipasavyo majukumu yao katika Skuli za Serikali ambazo
wameajiriwa.
“Tunazo
taarifa kwamba baadhi ya walimu wanatumika katika skuli binafsi na hivyo
utendaji wao unajikita zaidi katika Skuli hizo” Amesema Mh. Mmanga.
Awali
naibu katibu mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Abdalla Mzee
akitoa tathmini ya matokeo hayo amesema Skuli ya Chokocho ni miongoni mwa Skuli
tano za mwisho Zanzibar ambapo nne zipo Unguja.
Amesema
kati ya wanafunzi 42 waliofanya mtihani Skuli ya Chokocho ni wanafunzi 10 tu
waliofaulu na wengine 32 hawakufaulu. Akifafanua viwango vya ufaulu kwa
wanafunzi 10 amesema, mwanafunzi 1 tu
alipta daraja la pili, wanafunzi 2 walipata daraja la tatu na wanafunzi 7
walipata daraja la nne.
No comments:
Post a Comment