Habari za Punde

Ligi Daraja la pili Taifa Pemba, New Fighter yailaza New Version 4-3 katika hatua ya nne bora

 MCHEZAJI wa Timu ya New Fighter Abdull Khalifa akitafuta njia ya kuwapita wachezaji watatu wa timu ya New Version, wakati wa mchezo wao wa ligi hatua ya nne bora, New Fighter imeikuba na ushindi wa bao 4-3.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).

MCHEZAJI wa Timu ya New Fighter Abdull Khalifa, akijaribu kupiga mpira mbele ya wachezaji watatu wa timu ya New Version, wakati wa mchezo wa ligi hatua ya nne bora Taifa, uliopigwa uwanja wa Gombani, New Fighter imeibuka na ushidni wa bao 4-3.(PICHA NA ABDI SULEIMAN, PEMBA).

NA ABDI SULEIMAN, PEMBA

TIMU ya New Fighter imefanikiwa kumaliza ligi hatua ya nne bora daraja la pili Taifa Pemba, kwa ushindi wa bao 4-3 dhidi ya timu ya New Version.

Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa michezo Gombani, huku ukishuhudiwa na mashabiki wengi wa soka kutoka maeneo ya Wete na Kengeja, huku ukitumbuizwa na ngoma ya mdundiko kutoka Wete na Kengeja.

New Fighter ilianza kuzifumania nyavu za wapinzani wao dakika ya kwanza ya mchezo, kupitia kwa Abdull Khalif, bao la pili likifungwa na Ali Abdalla dakika ya nane.

Kuingia kwa mabao hayo New Version iliweza kujititimua na kuanza kusawazisha mabao hayo, kupitia kwa Bakari Ali dakika ya 29 na 40, hali iliyoamsha hamasa kwa mashabiki wa timu hiyo, kila dakika zikienda New Fighter iliweza kupata bao la tatu kipitia kwa Ali Abdalla dakika ya 42 mabao yaliyopeleka timu hizo mapumziko.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa uwanjani hapo, huku New Version ikiutawala vyema mchezo huo katika kipindi hicho, Khatib Sabri dakika ya 50 aliweza kuisawazishia timu yake bao la tatu uwanjani hapo.

Hata hivyo Abdalla Ali aliweza kuandika timu yake ya New fighter bao la nne dakika ya 65, huku Bakari Ali wa New Version akikosa Penanti ya wazi baada mlinda mlango wa New Fighter Ali Saleh Suleima.

Katika mchezo wa mchana Timu ya Maji Makali imechelewa kufika uwanjani, hali iliyowafanya waamuzi wa mchezo huo Asaa Ali kulivunja pambano hilo.

Maji makali ilifika uwanjani saa nane na nusu za mchana, huku wapinzani wao Eleven Star waliwasili mapema uwanja hapo tokea saa saba na nusu, wakiwasubiri maji makali kuchuana uwanjani hapo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.