Na Salmin Juma , Pemba
Jeshi la Polisi mkoa wa kusini Pemba
linamshikilia kijana wa miaka 16 mkaazi wa Gombani ya kale baada ya kudaiwa kumlawiti mtoto mdogo
wa kiume wa miaka ( 10 ) ambae pia ni mwanafunzi wa darasa la pili na
kumsababishia maumivu makali.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake madungu chakechake kamanda wa Polisi mkoa wa kusini Pemba Shehan Mohd Shehan alisema tukio hilo
limetokea jana majira ya saa 7:30 mchana huko Gombani ya Kale baada ya
mashuhuda kubaini unyama huo.
Alisema mtoto huyo aliagizwa na mamaake kwenda kununua stika zake za mabuku na alipokua
akirejea kijana huyo alimkamata kwa
nguvu na kumfunga mikono kisha kuanza kumalawiti.
“alimkamata kwa nguvu na kumpeleka
vichakani, akamfunga mikono, kisha alianza kumlawiti “ alisema Kamanda Shehan.
Kamanda Shehan alisema baadhi ya watu
walisikia sauti za kelele kizitoka porini , walipoamua kwenda na ndipo
kulipofanikisha kukamatwa kwa kijana huyo ingawa alijaribu kukimbia.
Shehan alisema, daktari amethibitisha
kuwa mtoto huyo alilawitiwa , hivyo jeshi la Polisi linaendelea kukamilisha
taratibu za kisheria ili kumfikisha mahakamani kijana huyo na sheria ichukue
mkondo wake.
“hatutomuachia kwasababu amefanya
kitendo cha kinyama sana, jeshi la
polisi mkoa wa kusini Pemba linalaani kwa nguvu zote juu ya tukio hili “
alisema kamanda
Kwaupande wake baba mzazi wa mtoto
huyo (jina linahifadhiwa) alisema ,
amehuzunishwa sana na tukio na hasa kuwa aliyetendewa tendo hilo ni mtoto wake
wa kwanza .
“taarifa nilipata nikiwa wete ,
mkewangu mmoja yupo huko, mamaake huyu alinipigia na kunipa taarifa hii,
niliumia sana , nilitoka mbio mpaka nyumbani
na kushuhudia hali hii “ alisema baba huyo.
Akizungumza kwa masikitiko huku
akiangua kilio mbele ya waandishi wa habari baba huyo alisema, wazee wa
mtuhumiwa wanamtumia rafiki yake ili amshawishi akubali mazungumzo na
kuyamaliza kienyeji jambo ambalo alisema halitaki na hayupo tayari kufanya
hivyo na anachotaka ni kuona sheria inachukua mkondo wake.
Nae Ust Rashid Ali Rashid wa Ole Kichoni alipoulizwa na mwandishi wa habari hizi juu ya
vipi uislamu unavyolizungumzia suala la
liwati alisema, jambo hilo
limeharamishwa katika uisilamu na haitakiwi kabisa hivyo kwa yoyote mwenye
kufanya tendo hilo ajue kuwa anafanya jambo baya ambalo Mungu lina mkasirisha.
“haifai kwa muislamu kumfanyia
mwenzake liwati wala kumbaka, wito wangu kwa wananchi wajiepushe na matendo haya
kwani athari yake ni kubwa kimwili na
hata kiakili, jamii ibadilike “ alisema Ust Rashid
No comments:
Post a Comment