Habari za Punde

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa CCM Taifa Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Akipokea Ripoti ya Uhakiki wa Mali za CCM.Katibu Mkuu Mpya wa CCM Alipotangazwa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli akiwa na Rais wa zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Visiwani) Dkt. Ali Mohamed Shein wakiwa na 'mlima' wa makabrasha ya ripoti ya uhakiki wa mali za chama baada ya kukabidhiwa na tume aliyounda kuchunguza mali hizo ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam
Wa kwanza kushoto ni Dkt Bashiru Ali Kakurwa ni Mwenyekiti wa Tume iliyoundwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli kuchunguza na kuhakiki mali za CCM akiwa na wajumbe wa tume hiyo mara tu baada ya jina lake kupendekezwa kuchukua nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM mbele ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam
Wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya  CCM wakisamama na kuunga mkono kwa kauli moja pendekezo la Dkt. Bashiru Ali Kakurwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa CCM ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Tume iliyoundwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Dkt John Pombe Magufuli kuchunguza na kuhakiki mali za CCM  Dkt. Bashiru Ali Kakurwa akipongezwa  na wajumbe wa tume hiyo mara tu baada ya jina lake kupendekezwa kuchukua nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM mbele ya wajumbe wa Mkutano wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho ukumbi wa Kikwete jijini Dar es salaam Mei 29, 2018
Picha na Ikulu.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.