Habari za Punde

WASAIDIZI WA MAKAMU WA RAIS WATOA FUTARI KWA WATOTO YATIMA WA KITUO CHA RAHMAN DODOMAWasaidizi wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wametoa futari kwa kituo cha watoto Yatima cha Rahman kilichopo Chang’ombe Dodoma.
Kituo hicho chenye watoto 120 ambao kati ya hao 75 ni yatima ambapo hupatiwa Elimu ya Dini na Lugha.
Wasaidizi hao ambao waliwakilishwa na Kaimu Katibu wa Makamu wa Rais Bi. Maulidah Hassan na Msaidizi wa Masula ya Siasa Ndugu Nehemia Mandia kwa pamoja walisema imekuwa utamaduni wao kukutana, kuzungumza na kusaidia watoto yatima, watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu na walemavu na wameahidi kuendelea kusaidia kila inapowezekana.
Nae mwanzilishi wa Kituo hicho Bi. Rukia Hamisi ameshukuru kwa wasaidizi wa Mheshimiwa Makamu wa Rais kufika ofisini kwake na ameomba Mheshimiwa Makamu wa Rais akipata nafasi naye afike kituoni kwani watoto wanampenda sana pili alishukuru kwa futari.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.