Habari za Punde

Matukio ya Ajali Barabara ya Fuoni Zanzibar.

Wananchi katika eneo la barabara ya Fuoni wakiangali ajali ya gari yenye namba za usajili Z228GL, iliyokuwa imeegesha kando ya barabara hiyo na kuingia katika mtaro ulioko katika barabara hiyo, ajali hiyo imesababishwa na gari yenye namba za usajili Z807 GM ikitokea fuone ikielekea mjini, katika ajali hiyo hakuna Mtu aliyefariki na kujeruhiwa.
Gari yenye namba za usajili Z228 GL ikiwa katika mtaro wa maji machafu kando ya barabara hiyo baada ya kugongwa kwa nyumba ikiwa imeegeshwa katika barabara hiyo.

Gari yenye namba za usajli Z807 GM ilioacha njia na kuligonga gari lilikowa limeegeshwa kando ya barabara hiyo ya fuoni na kuacha njia na kugonga gati la nyumba jirani na barabara hiyo.


No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.