Habari za Punde

DK. KIGWANGALLA AHITIMISHA MAADHIMISHO YA KITAIFA YA KIMONDO DUNIANI MKOANI SONGW

Na Hamza Temba-Songwe.
................................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ametoa wito kwa wadau wa utalii wa Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kuweka juhudi za pamoja na kushirikiana na Serikali katika kuendeleza na kutangaza vivutio vya utalii vya kanda hiyo ili viweze  kunufaisha zaidi wananchi na Taifa kwa ujumla.

Ametoa wito huo jana wakati akihitimisha kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani ambayo kitaifa yamefanyika katika eneo la Kimondo cha Mbozi kwenye kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi mkoani Songwe.

Amesema mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ina vivutio vingi vya utalii ambavyo bado havijaendelezwa vya kutosha na kutangazwa vizuri kama vile vya nyanda ya kaskazini ikiwemo vivutio vya mambo ya kale, wanyamapori na tamaduni mbalimbali.

Amesema mpango wa Serikali wa maendeleo wa miaka mitano umeelekeza kuwepo kwa shughuli za utalii zitakazoenda sambamba na kuinua maisha ya wananchi, hivyo ametoa rai kwa idara ya mambo ya kale na utalii, na taasisi za wizara yake kushirikiana na uongozi wa mkoa wa Songwe  kupanga namna ya kuendeleza eneo la kimondo cha Mbozi kwa kuanzisha shughuli mbalimbali za kiuchumi zitakazowainua wananchi wa eneo hilo kupitia utalii.

Amesema Serikali kupitia Wizara yake imeanza kuchukua hatua ya kufungua utalii wa kanda hiyo ambapo imesaini mkataba wa mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia kwa ajiri ya Mradi wa Kusimamia maliasili na Kuendeleza Utalii Kanda ya Kusini (REGROW).

Pamoja na kanda hiyo amesema Serikali pia inafungua utalii wa kanda ya Kaskazini Magharibi ambapo tayari mapori matano ya akiba yameshatangazwa kupandishwa hadhi ya kuwa Hifadhi za Taifa, huku ujenzi unaendelea wa uwanja wa ndege wa kisasa wa Chato ukitarajiwa kuchagiza maendeleo ya hifadhi hizo.

Dk. Kigwangalla pia ametoa wito kwa wadau wa kanda hizo kutumia fursa hizo kuwekeza katika sekta ya utalii ikiwemo ujenzi wa mahoteli ya kitalii, biashara ya kusafirisha watalii na huduma nyingine mbalimbali katika sekta hiyo.

Katika hatua nyingine, Waziri Kigwangalla amezindua maonesho ya utalii ya Karibu Kusini ambayo yatafanyika mwezi Spetemba mkoni Iringa ambapo ametoa wito wa wananvhi wa mikoa hiyo kuhudhuria kwa wingi waweze kujifunza na kuona mambo mbalimbali ya sekta hiyo.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga amesema wizara yake inaendelea na mikakati mbalimbali ya kutangaza vivutio vya utalii nchini ambapo mwezi Septemba kila mwaka utakuwa na mwezi maalum wa kuadhimisha utamaduni wa Mtanzania ili kukuza utalii wa kiutamaduni.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa amesema mkoa wake umedhamiria kutangaza vivutio vya utalii mkoani humo kupitia njia za matamasha, michezo mbalimbali na kuwashirikisha wadau. 
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (katikati), Naibu Waziri wake, Japhet Hasunga (kushoto kwake), Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Galawa (kulia kwake) na viongozi wengine mkoani humo wakiangalia Kimondo cha Mbozi wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ndolezi wilaya Mbozi mkoani Songwe wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kuhusu Kimondo cha Mbozi kutoka kwa mkuu wa kituo hicho, Mhifadhi wa Mambo ya Kale, Filmerick Basange wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wake, Japhet Hasunga na Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Galawa.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akinasisha sumaku kwenye Kimondo cha Mbozi wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. Kutoka kushoto nyuma yake ni Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Galawa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chuku Galawa wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. Wa tatu kushoto Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Naibu Waziri wake, Japhet Hasunga na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa wakijaribu kahawa ya asili inayozalishwa mkoani humo kwenye maonesho wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi jana.
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Naibu Waziri wake, Japhet Hasunga na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa wakijaribu maziwa ya mtindi yanayozalishwa mkoani humo kwenye maonesho wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi jana. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa wakishiriki kucheza ngoma wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, akipata maelezo kuhusu vinyago vya kiutamaduni vinavyoelimisha jamii kutoka kwa mmoja ya waoneshaji wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wake, Japhet Hasunga na Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa (kulia kwake). 
 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na wananchi wakati wa kuhitimisha maadhimisho hayo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Naibu Waziri wake, Japhet Hasunga (kushoto kwake), Mkuu wa Mkoa wa Songwe (kulia kwake), Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela na viongozi wengine wakishiriki kukata utepe kama ishara kuzindua maonesho ya Karibu Kusini yatakayofanyika mwezi Septemba mwaka huu, mkoani Iringa wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa cheti maalum cha wizara cha kutambua mchango wake wa kuhamasisha na kuendeleza shughuli za utalii mkoani humo. Kushoto anaeshuhudia ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Japhet Hasunga.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na Naibu Waziri wake, Japhet Hasunga wakinyoosha mikono huu kama ishara ya kuwakaribisha wananchi katika maonesho ya Karibu Kusini yatakayofanyika mwezi Septemba, mkoani Iringa mda mfupi baada ya kuyazindua wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Kimondo Duniani yaliyofanyika katika kijiji cha Ndolezi wilaya ya Mbozi mkoani Songwe jana.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.