Habari za Punde

Kampeni Valisha Mtoto Viatu "A Pair For Every Child Camping"# PEC Campaign.

Mradi wa Best of Zanzibar unaofadhili Kampeni ya "Valisha Mtoto Kiatu" kwa Wanafunzi wa Skuli za Kijini na Mbuyu Tende Kijiji cha Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakiendelea na zoezi hilo kwa Wanafunzi wa Skuli hizo kutoa viatu kwa Wanafunzi, lengo la Mradi huu kutowa huduma hiyo kwa Wanafunzi wa Wote wa Zanzibar kupitia Mradi huo wa Kampeni ya "Valisha Mtoto Viatu" .
CSR Program Maneja Aminata Keita akizungumza wakati wa kampeni hiyo ya Valisha Mtoto Viati iliofanyika katika Skuli ya Sekondari na Msingi Kijini Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja, wakati wa kampeni hiyo ya kugawa viatu kwa Wanafunzi wa Skuli hizo, wakiendelea na kampeni hiyo.
Mratibu wa Elimu na Uwezeshaji Mradi wa Best of Zanzibar Ndg. Ali Suleiman, akimvisha mmoja wa Mtoto wa Skuli ya Msingi Kijini Viatu wakati wa kampeni hiyo ya "Valisha Mtoto Viatu" inayofadhiliwa na Kampuni ya Pennyroyal kupitia Mradi wake wa Best of Zanzibar, kutowa huduma hiyo wa kuagawa Viatu kwa Wanafunzi wa Skuli zote za Zanzibar. 
Wanafunzi wa Skuli ya Msingi na Sekondari Kijini Mkoa wa Kuzini Unguja Kijiji cha Matemwe wakifuarahia baada ya kukabidhiwa viata wakati wa Kampeni ya 'Valisha Mtoto Viatu"  inayofadhiliwa na Mradi wa Best Of Zanzibar 

Tarehe 11 April 2018, Best of Zanzibar ilifanya uzinduzi wa Kampeni yake ya Valisha Mtoto Viatu ambayo ilizinduliwa rasmi na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Vuai Ali Vuai, lengo kuu ni kuanza kuwavisha viatu wanafunzi wa skuli za Kijini na Mbuyu Tende ambao zaidi ya 60% wanaenda skuli bila viatu.

Skuli hizo mbili zina jumla ya wanafunzi 1,500 na baada ya uzinduzi wa Kampeni hiyo, wadau mbalimbali walijitokeza kuchangia kampeni hiyo ambapo hadi sasa karibia viatu 900 vimeshachangiwa, Best of Zanzibar inatoa shukrani za dhati kwa wadau mbali mbali ambao wamei-support kampeni hiyo ambayo kwa Kingereza inajulikana kama "A Pair for Every Child Campaign" na hashtag yake ni #PECcampaign

Awamu ya pili ya Valisha Mtoto Viatu imefanyika tarehe 26 -27 Juni 2018 katika Skuli ya Kijini Matemwe ambapo viatu zaidi ya 700 vimeanza kuvishwa kwa wanafunzi wa msingi na baadae Sekondari, Best of Zanzibar kwa kushirikiana na Walimu wa Kijini wamewavisha viatu wanafunzi hao pamoja na kuwaomba kuanzia sasa waweze kuvaa viatu hivyo wanapokuja shuleni.

Best of Zanzibar bado inaungana na kuwakaribisha wadau wote wa maendeleo na jamii kuungana nao katika kuwekeza katika elimu na kuwaomba pia kuwa Mabalozi wao wa Kampeni hii muhimu ya "Valisha Mtoto Viatu" Kwamba, kwa umuhimu wa kampeni hii na kwa kushirikiana na wadau mbali mbali, Best of Zanzibar inaazimia kuifanya kampeni hii Zanzibar nzima kwa skuli za Vijijini kwani ndio wanafunzi wengi wanaenda bile viatu.

Tunashukuru kwa wote waliotuunga mkono na tumeanza kupata Mabalozi kutoka ndani na nje ya Zanzibar kwa Kampeni hii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.