Habari za Punde

Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Ngoma Aanza Matibabu Nchini India.


NEWS ALERT: MGUNDUZI WA MADINI YA TANZANITE MZEE JUMANNE NGOMA AANZA MATIBABU INDIA

Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Mzee Jumanne Mhero Ngoma, ambaye anasumbuliwa na maradhi ya kupooza mwili,  leo amenza rasmi matibabu katika Hospitali ya Apollo jijini New Delhi nchini India.

Kwa mujibu wa binti yake, Bi. Asha Ngoma, mgunduzi huyo ameamua kusaka matibabu zaidi  baada ya kufanyiwa matibabu hapa nchini ili kuona kama anaweza kupona kwa uharaka zaidi.

“Mzee amekuwa akipatiwa matibabu tokea wakati ule Rais Magufuli  alipomzawadia pesa shilingi milioni 100 mwezi wa Aprili mwaka huu  ya matibabu wakati  uzinduzi wa ukuta unaozunguka machimbo ya madini Mirerani mwezi April mwaka huu.

“Tunamshukur sana Rais Magufuli kwani pesa hiyo tulipewa mara moja nasi tukaanza matibabu hapo nyumbani  na kwa kweli amemsaidia sana sana  na hapa India tunatarajia matibabu haya ya ziada yatamsaidia zaidi”, alisema Bi. Asha ambaye ameongozana  na mjukuu wa Mzee Ngoma, Khalifa.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.