Habari za Punde

Taasisi za kifedha zaombwa kutenga fedha kwa watu wenye ulemavu

Na Takdir Ali,                                                  
Taasisi za kifedha zimeombwa kutenga fungu maalum kwa watu wenye ulemavu ili waweze kufaidika na fursa hiyo.
Amesema Mashirika ya kifedha kama vile Benki wameweka Bajeti maalum kwa ajili ya kuasidia mambo ya kijamii lakini Watu hao wamekuwa hawaipati hivyo ni vyema kuainisha asilimia maalum ili na wao waweze kufaidika na Msaada huo kama walivyo Wayu wengine.
Akizungumza na Waandishi wa Habari huko Ofisini kwake Kikwajuni Wilaya ya Mjini Mratibu wa mradi wa kuwawezesha kiuchumi Watu wenye Ulemavu katika Umoja wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar (U W Z) Muhammed Abdallah Muhammed amesema wamekuwa hawafaidiki na misaada inayotolewa jambo ambalo linapelekea kujihisi wanatengwa na jamii.
Amesema kitendo hicho kinatoa taswira mbaya kwa Watu hao na endapo haitorekebishwa lengo la Serikali la kuwanyua Wananchi wake kiuchumi halitoweza kufikiwa hasa kwa Watu wenye Ulemavu.
Ameeka wazi ya kuwa Watu hao ni sawa na Watu wengine katika jamii hivyo ni vyema kupewa kipao mbele katika fursa zinazotolewa kwani wanahaki sawa kama Watu wengine.
“Baadhi ya Watu wenye Ulemavu wanaishi katika mazingira magumu tena sana,wanashindwa hata kupata mlo mmoja kwa siku.”Alisema Mratibu huyo.
Hata hivyo amesema umefika kwa Wanajamii kushirikiana katika kuhakikisha Watu wenye Ulemavu wanapewa nyenzo za kuendeshea maisha yao kiwemo miradi ya kimaendeleo ili waweze kujipatia kipato cha kuendesha maisha yao na kuepukana na hali tegemezi.
Muhammed ambae pia ni Afisa Ufuatiliaji na Tathmini katika Umoja wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar amesema bado tatizo la Umasikini linawakabili kwa kiasi kikubwa licha ya miradi mbali mbali wanayoianzisha katika maeneo yao.

Amefafanua kuwa Umoja wa Watu Ulemavu umeweka Mikakati ya kuhakiakisha wanawawezesha Watu wenye Ulemavu kujikwanua na balaa hilo kwa kuwapa Mafunzo ya Ujasiriamali na kuwaanzishia miradi ya kimaendeleo katika maeneo ya Mjini na Vijijini.
Vikundi vinavyojengewa uwezo na Umoja wa Watu wenye Ulemavu Zanzibar (UWZ) Vikundi vya Ufinyanzi,Ufumaji. Ufugaji, Kilimo na Biashara.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.