Habari za Punde

Wasanii Mbalimbali wa Zanzibar Wakishiriki katika Maandamano ya Uzinduzi wa Tamasha la 23 la Mzanzibar Katika Viwanja Vya Mapinduzi Square Michezani Zanzibar.

Maandamano ya Uzinduzi wa Tamasha la 23 la Mzanzibar katika viwanja vya Mapinduzi Square Michezani, wasanii wakiingia katika viwanja hivyo kwa ajili ya Uzinduzi wake uliofanywa na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Mahmoud Thabit Kombo kwa niaba ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi.  
Wasanii wa Ngoma ya Kilua wakishiriki katika maandamano ya maonesho ya Uzinduzi wa Tamasha la 23 la Mzanzibar katika viwanja vya Mapinduzi Square Michezani.
Mwananchi akionesha jinsi ya matumizi ya Mzegazega uliokuwa ukitumika kwa kuuzia maji majumbani akionesha Utamaduni huo uliokuwa ukitumika na Wazee wa zamani Visiwani Zanzibar.
Mwananchi akiwa na dele la kahawa la shaba lililokuwa likitumika kuuzia kahawa mitaa enzi hizo.
Wananchi wakionesha jinsi ya kumshikikiza biarusi nyumbani kwake akiwa amivunikwa kwa Baibui la ukaya lililokuwa likitumiwa na Wazee wetu zamani kwa sasa Baibui aina hii ni aghlabu kuliona kuvaliwa na Vijana Zanzibar. Wakionesha Utamaduni huo wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Mzanzibar.
Wananchi wakionesha vifaa vya matumizi ya nyumba Vungu na vyetezo vilivyotengenezwa kwa udogo, wakionesha Utamaduni huo wakati wa Tamasha la 23 la Mzanzibari katika viwanja vya Mapinduzi Square Michezani Zanzibar.
Wananchi wakiwa na Mitungi, Kata za vifuu, Vyetezo, Mikungu ya Tanu iliotengenezwa kwa udogo, vifaa hivi vilikuwa vikitumika enzi za wazee wetu wa Visiwa vya Unguja na Pemba. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.