Habari za Punde

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu Awapongeza Mashujaa 70 Waliopanda Mlima Kilimanjaro Kwa Lengo la Kuchangia Fedha za Mapambano Dhidi ya Ukimwi.

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto ,Ummy Mwalimu akiwa ameongozana na viongozi wengine wakiwemo Mkuu wa mkoa wa Geita,Robert Gabriel (mwenye kofia) Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Kippi Warioba (kushoto kwake) na kulia kwa Waziri ni Makamu wa Rais wa Kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Geita wakati wa mapokezi  ya Mashujaa 45 waliopanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za Mapambano Dhidi ya UKIMWI.
Sehemu ya Washiriki wa Changamoto ya kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za Mapambano Dhidi ya UKIMWI kupitia Kampeni ya Kili Challenge.
Washiriki wengine katika kampeni hiyo wametumia Baiskeli kuzunguka Mlima Kilimanjaro.
Kiongozi wa wapandaji ,Bw Moses kutoka mgodo wa Dhahabu wa Geita akipokelewa na Waziri wa Afya,Ummy Mwalimu mara baada ya kushuka kutoka katika kilele cha Uhuru.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto ,Ummy Mwalimu  akizungumza wakati wa Hafla fupi ya mapokezi ya Mashujaa hao iliyofanyika katika lango la Mweka .
Mkuu wa mkoa wa Geita,Robert Gabriel akizungumza wakati wa hafla hiyo mara baada ya kuwapokea Mashujaa hao.
Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS ) Dkt Leonard Maboko akizungumza wakati wa Hafla hiyo. 
Mgeni rasmi katika Hafla hiyo  Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto ,Ummy Mwalimu akikabidhi vyeti kwa washiriki wa changamoto hiyo waliofanikiwa kufika katika Kilele cha Uhuru.
Makamu wa Rais wa Kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Geita ,(GGM) Simoni Shayo akifungua Champagne wakati wa hafla hiyo. 
Makamu wa Rais wa GGM ,Simon Shayo akimimina wine katika Bilauli ya Waziri wa Afya ,Ummy Mwalimu .
Makamu wa Rais wa GGM ,Simon Shayo akimimina wine katika Bilauli ya Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro ,Betrita Loibook .
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa zoezi la kupanda Mlima.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa zoezi la kuzunguka Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini .
SERIKALI imeanza majaribio ya kutoa Dawa za miezi Mitatu hadi sita kwa watu wenye Maambukizi ya Virusi vya Ukimwi na kwamba mwakani imepanga kutoa Dawa zenye ubora na ufanisi zaidi mara baada ya Dawa zinazotumika sasa kumalizika.

Mwanzo wa mwaka 2005 hadi sasa , idadi ya watu Wanaoishi na Virusi vya Ukimwi na wale wanaokufa kutokana na ugonjwa huo nchini inatajwa kupungua, huku takwimu zikionesha mafanikio yanayotokana na juhudi zinazofanywa na Serikali kupitia Tume ya kupambana na UKIMWI  Tanzania (TACAIDS), Wizara ya afya, asasi zisizo za kiserikali na jamii kwa ujumla.

Hata hivyo endapo juhudi hizi hazitaongezeka, hatari ya ugonjwa huo kuleta madhara bado itakua kubwa na hili ndilo linawaasukuma Mashujaa zaidi ya 70 kushiriki kampeni Dhidi ya Ukimwi kwa kupanda Mlima Kilimanjaro ijulikanayo kama Kili Challenge.

Mashujaa hao walioianza safari ya kupanda Mlima huo kupitia njia ya Machame wakiwemo waendesha Baiskeli wamerejea na kupokelewa na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto ,Ummy Mwalimu  na kutangaza Habari njema.

Waziri Mwalimu akaeleza kuwa lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inafikia malengo makuu matatu ifikapo mwaka 2020 likiwemo la angalau asilimia 90 ya atu wanaoishi na maambukizi ya Virusi  vya UKIMWI  na UKIMWI wajue kwamba wana maambuziki .

Mkurugenzi wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS ) Dkt Leonard Maboko ameipongeza kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Geita (GGM) kwa kuratibu zoezi hilo la kuchangisha fedha kwa ajli ya Mapambano Dhidi ya Ukimwi huku akitoa hamasa kwa wadau wengine kujitokeza katika kuchangia fedha kwa ajili ya Mapambano hayo.

Katika safari ya Kupanda Mlima Kilimanjaro na kuuzunguka kwa kutumia Baiskeli,Washiriki 40 kati ya 45 waliopanda ndio waliofanikiwa kufika katika kilele cha Uhuru miongoni mwao wakiwa ni Vijana wanne kutoka kituo cha Moyo wa Huruma cha mkoani Geita.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.