Habari za Punde

Kongamano la Kumpongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli Kufanyika Augusti 31, 2018 Jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Taasisi ya Nuru ya Taifa Tanzania, Gadiell Joseph, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi, kuhusu kongamano la kumpongeza Rais Dk.John Pombe Magufuli kutokana na utendaji wake kazi mzuri katika kuliongoza Taifa la Tanzania.
Mwenyekiti wa Taasisi ya Nuru ya Taifa Tanzania, Gadiell Joseph, akisisitiza jambo kwenye mkutano huo wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.

Na Dotto Mwaibale
KONGAMANO la kumpongeza Rais Dk.John Pombe Magufuli kutokana na utendaji kazi wake mzuri linatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa Taasisi ya Nuru ya Taifa Tanzania, Gadiell Joseph alisema awali kongamano hilo lilikuwa lifanyike Agosti 25, 2018 lakini wakalazimika kuliahirisha kutokana na Rais Magufuli kufiwa na dada yake.

"Kongamano hilo lililkuwa lifanyike Agosti 25, 2018 lakini kutokana na msiba huo mkubwa tumelazimika kulisogeza mbele hadi tarehe 31" alisema Joseph.

Joseph alisema kongamano hilo litafanyika ukumbi wa Karimjee kuanzia saa tatu asubuhi.

Alitaja baadhi ya mambo makubwa ambayo yamefanywa na Rais Magufuli kwa kipindi kifupi ambacho amekaa madarakani kuwa ni kupambana na ufisadi, ujenzi wa barabara za juu, kutoa elimu bure, huduma za afya, ununuzi wa ndege na kuboresha miradi mbalimbali.

Kongamano hilo limeandaliwa na Taasisi ya Nuru ya Taifa Tanzania.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.