Habari za Punde

Mkoa wa Morogoro Wajipanga Kuongeza Uzalishaji wa Zao la Korosho.


KATIBU Tawala Msaidizi anayesimamia sekta ya uchumi na uzalishaji ofisi ya mkuu wa mkoa mkoa wa Morogoro Ernest Mkondo akizungumza kuhusiana na mpango wao wa kuongeza uzalishaji wa zao la Korosho wakati wa ziara ya viongozi wa  bodi Korosho nchini ilipokutana na wakulima wa korosho wa wilaya za Morogoro, Ulanga, Malinyi, Kilosa, Mvomero, Gairo mkoani Morogoro na kutoa elimu namna bora ya wakulima wanaweza kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia kilimo bora

Afisa Kilimo wa Bodi ya Korosho Tanzania Frank Mfutakamba kulia akimsikiliza mmoja wa wakulima wa zao la Korosho mkoani Morogoro mara baada ya kuwatembelea wakulima na kutoa elimu namna bora ya wakulima wanaweza kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia kilimo bora
KATIBU Tawala Msaidizi anayesimamia sekta ya uchumi na uzalishaji ofisi ya mkuu wa mkoa mkoa wa Morogoro Ernest Mkondo kushoto akiagana na Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Tanzania Bryson Mshana mara baada ya kufanya mazungumzo naye.
Afisa Uhusiano wa Bodi ya Korosho Tanzania Bryson Mshana kulia akisalimiana na wakulima wa zao la Korosho mkoani Morogoro mara baada ya kuwatembelea  na kutoa elimu namna bora ya wakulima wanaweza kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia kilimo bora


Na, Mwandishi Wetu. Morogoro.
KATIBU Tawala Msaidizi anayesimamia sekta ya uchumi na uzalishaji ofisi ya mkuu wa mkoa mkoa wa Morogoro Ernest Mkondo amesema mkoa huo umejipanga kufanya uhamasishaji na ufuatiliaji wa zao la Korosho ili kuhakikisha uzalishaji unaongezeka kuliko iliyokuwa miaka iliyopita

Mkondo aliyasema hayo wakati wa bodi Korosho nchini ilipokutana na wakulima wa korosho wa wilaya za Morogoro, Ulanga, Malinyi, Kilosa, Mvomero, Gairo mkoani Morogoro na kutoa elimu namna bora ya wakulima wanaweza kuongeza uzalishaji kwa kuzingatia kilimo bora

Ambapo alisema uhamasishaji huo utashirikishi wakuu wa wilaya na viongozi wengine wa ngazi za chini kwa lengo la kuhakakikisha kilimo hicho kinalimwa kwa tija kubwa ili kuweza kuwasaidia kuwainua wakulima kiuchumi..

Alisema licha ya kwamba wana wataalamu wana upungufu mkubwa wa wataalamu wa kilimo kwenye maeneo ya vijijini wakati wanawasubiri wanachofanya wamewagawa wa maeneo ya kata na Vijiji ili kuwasaidia kuongeza nguvu kutoa ushauri wa ugani kwa wakulima “Anasema

Aidha alisema hivi sasa wanawahimiza wataalamu waliopo ngazi za kata wafike kwenye maeneo ya vijiji kutoa ushauri hasa mashamba darasa hilo litasaidia kutoa elimu inayohusika kwenye mazao mbalimbali ikiwemo zao la korosho.

Mkondo alisema wanalifanya hilo kwa kushirikiana na bodi ya Korosho na maafisa ugani ambao hawajapata elimu juu ya uzalishaji huo wanaitwa na kupewa elimu juu ya zao husika ili waweze kujua namna ya kuwaelimisha wakulima.

Akizungumzia suala la malipo yanayofanywa na bodi ya korosho alisema licha ya kuwepo kwa changamoto lakini wamehaidi kuanza kuyashughulikia kwa kuanza kufanya uhakiki ili waweze kujua vikundi vipi vimezalisha na baadae waweze kulipwa malipo halali.

“Lakini kama uhakiki umekwisha kufanyika bodi ya korosho na umekamilika malipo yafanyike kwa wakati ili vikundi viweze kulipwa kwa haraka huku akisisitiza kwamba pembejeo zinasambazwa na serikali kupitia bodi ya Korosho hivyo wakulima wafuatwe taratibu zilizopo waweze kupata pembejeo hizo”Anasema

Aliongeza kuwa mwaka jana mkoa huo uliweza kustawisha vitalu 36 vya korosho ambavyo walipata miche 702,000 ilioteshwa na vikundi mbalimbali vilivyopata msaada kutoka bodi ya Korosho lakini waliweza kupata mbegu za kupanda kilo 4154.

Alisema baada ya kupata mbegu hizo waliweza kusambazwa na kupandwa na wakulima kutokana na uhamasishaji katika mkoa kuwa mkubwa zaidi kama kutokana na wananchi kuitikia mwitikio mzuri wa kuweza kulima zao hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.