Habari za Punde

UN Women Kuendelea Kutoa Msaada Kwa Wanawake Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Wanawake (UN Women), Phunzile Mlambo- Ngcuka, akisalimiana na wanawake wajasiriamali baada ya kuwasili viwanja vya Soko la Mchikichini, Ilala jijini Dar es Salaam juzi kwenye sherehe ya mafanikio ya mradi wa 'Mpe Riziki si Matusi' ambapo alikuwa ni mgeni rasmi. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita.
 Wanawake wajasiriamali wakiwa na Mkurugenzi huyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, akimpa Bi. Mlambo zawadi ya Khanga.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, akiteta jambo na Bi. Mlambo.
 Kundi la Sanaa la Nimujo, likitoa burudani.
 Wasanii wakundi hilo wakiigiza.
 Mwezeshaji wa kisheria masokoni, Consolatha Cleophas, akitoa ushuhuda mbele ya mgeni rasmi.
  Mwezeshaji wa kisheria Soko la Tabata Muslim, Aisha Juma, akitoa ushuhuda mbele ya mgeni rasmi.
 Mwenyekiti wa Soko la Temeke Stereo, Omary Mangilile, akizungumza katika hafla hiyo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Equality for Growth (EfG), Jane Magigita, akihutubia kwenye sherehe hizo.
 Bi.Mlambo akihutubia.
 Picha ya pamoja na mgeni rasmi.
 Picha ya pamoja.


 Sherehe ikiendelea.
 Mgeni rasmi akiserebuka sanjari na Mkurugenzi wa EfG, Jane Magigita.
 Hapa mgeni rasmi akisalimiana na wanawake wajasiriamali.



Wanawake wajasiriamali wakiwa na mabango yao.

Mgeni rasmi akiaga wakati akiondoka katika viwanja hivyo.

Na Dotto Mwaibale
MKURUGENZI Mtendaji wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia Wanawake (UN Women), Phunzile Mlambo- Ngcuka, amesema umoja huo utaendelea kuwasaidia wanawake wa Tanzania.

Mlambo ambaye alikuwa mgeni rasmi aliyasema hayo kwenye sherehe ya mafanikio ya mradi wa 'Mpe Riziki si Matusi' zilizofanyika viwanja vya Soko la Mchikichini, Ilala jijini Dar es Salaam ambao unasimamiwa na Shirika la Equality for Growth (EfG).

"Tutaendelea kuwasaidia wanawake wa Tanzania katika maeneo mbalimbali lakini pia napenda kuwapongeza kwa hatua mliyoifikia kupitia mradi huu na kuwa na moyo wa kupenda kuyapeleka mafanikio mliyopata kwa wanawake wenzenu jambo ili limenifurahisa sana" alisema Mlambo.

Katika hatua nyingine Mlambo aliwaomba wanaume kuendelea kuthamini mchango wa wanawake ili kuwatia nguvu badala ya kuwabeza kwani kazi wanayoifanya ni kubwa.

Mkurugenzi wa EfG, Jane Magigita alisema hivi sasa matukio ya ukatili wa kijinsia yamepungua kwa asilimia 81 hasa lugha za matusi na bughudha kwa wanawake.

Alisema utafiti uliofanywa na EfG Desemba 2017 umeonesha asilimia 92 ya wanawake wako huru kufanya biashara, 89 kupata haki za kiuchumi, 70 kugombea na kushika nafasi mbalimbali za uongozi, 83 kufanya maamuzi na 91 kupata huduma za msaada pindi wanapofanyiwa ukatili.

"Hivi sasa wanawake katika uongozi wa masoko wameongozeka kutoka asilimia 14 mpaka 26 na tuna mwenyekiti mwanamke katika Soko la Kiwalani na pia katika masoko mengine, uongozi wa soko ni asilimia 50/50," alisema Magigita. 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.