Habari za Punde

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya amali awapongeza wanafunzi waliofanya vizuri katika mitihani ya kidato cha sita



Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma akiwa pamoja na mwanafunzi aliyeingia katika  wanafunzi kumi bora katika mtihani9 wa kidato cha sita

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Riziki Pembe Juma amewapongeza wanafunzi wahitimu wa kidato cha sita kwa kufanya vizuri katika masomo yao.

Mhe. Riziki alitoa pongezi hizo leo katika sherehe ya kuwapongeza wanafunzi wahitimu wa kidato cha sita wa skuli ya sekondari ya Lumumba. hafla ambayo ilifanyika katika ukumbi wa Skuli ya sekondari ya Lumumba.


Akizungumza katika hafla hiyo Mhe Waziri wa Elimu aliwataka wahitimu hao wasisahau wanakotoka na kuaanglia vyema wanakokwenda kwani safari ya kutafuta elimu ni ndefu sana hivyo wawe makini na wasikaribishe mambo ambayo wakati wake bado.

Pia aliwasisitiza kuwa wakaendelee kuwa wasomi wazuri huko chuoni. Hata hivyo aliendelea na kutoa pongezi kubwa sana kwa mwanafunzi Fahad Rashid Khamis kwa kuwa miongoni mwa wanafunzi kumi (10) bora Tanzania na kumtaka aendelee vizuri huko mbeleni anakoendelea.

Aidha, aliwapongeza walimu kwa kuchukua juhudi zao binafsi hadi kufikia lengo walilolikusudia na kuwataka kujitahidi kutimiza majukumu yao na kuhakikisha malengo yanafikiwa kama yanavyotarajiwa.

Mwisho aliishukuru Jumuiya ya Green Light Foundation kwa misaada mbali mbali wanayoitoa katika kusaidia gurudumu la elimu liende mbele na kutoa wito kwa wadau wengine mbali mbali kusaidia katika sekta ya elimu ili kuweza kuwasaidia wanafunzi waweze kufanya vizuri katika mitihani yao.

Nae mwanafunzi Fahad Rashid Khamis aliwashauri wanafunzi wenzake wawe na ushirikiano katika masomo yao na wawasikilize walimu wao wakati wanapopatiwa elimu ili kuzidisha ufaulu wa wanafunzi maskulini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.